Ndege ya shirika la hifadhi la
taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa
mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa
Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.
Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda Mahamud Muhamed kasema ajali ilitokea juzi december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.
Ni ndege ya abiria mali ya
hifadhi ya taifa ya TANAPA na inauwezo wa kuchukua abiria wanne na
imeanguka umbali wa kilometa moja na nusu kutoka uwanja wa ndege.Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda Mahamud Muhamed kasema ajali ilitokea juzi december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.
Rubani wa ndege hiyo alipata msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa shamani mwao ambapo mmoja wao alisema wakati akiwa anafanya shughuli zake za kilimo ghafla aliona ndege angani ikizimika injini na muda mfupi baadae ikaanguka jirani na mti wa mwembe, kazi ya uokoaji ilichukua muda kidogo kutokana na nyuki.
No comments:
Post a Comment