Nahodha wa timu ya Zanzibar Hereos Nadir Haroub Kanavaro akiishukuru Serekali ya
Zanzibar kwa mashirikiano iliyotoa kwa timu hiyo.
Naibu Waziri wa Habari,Utamadu Utamaduni na Michezo Bi Hindi Hamadi akiwashukuru
wa wachezaji pamoja na viongozi wao kwa ushindi walio upata wa nafasi ya tatu
katika mashindano ya Challenge Uganda.
Na: Faki Mjaka Maelezo Zanzibar-
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imesema imefurahishwa sana na kiwango cha mchezo kilichooneshwa na Timu
ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) katika Mashindano ya Challenge licha ya
kuambulia mshindi wa tatu wa mashindano hayo.
Aidha katika kuipongeza
Timu hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed
Shein amepanga kukutana na Vijana hao ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo ya
kuimarisha kikosi cha Timu hiyo.
Naibu Waziri wa Habari
Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis ameyasema hayo ukumbi wa Hoteli
ya Bwawani wakati alipokuwa akizungumza na Timu hiyo mara baada ya kuwasili
Zanzibar kutoka Uganda.
"Naleta salamu Rasmi za
Serikali kwa juhudi kubwa mliyoifanya kule Uganda na Rais kasema atapanga siku
ya kukutana nanyinyi ili mbadilishane naye mawazo ya kuboresha timu zaidi"
alisema Bihidi.
Amesema juhudi ambazo
zilioneshwa na Vijana wa Zanzibar Heroes zinafaa kuthaminiwa kutokana na kucheza
na timu ziliozojaa uzoefu na wachezaji maarufu lakini vijana hao walipigana
kiume na kuambulia nafasi ya tatu.
Bihindi amewataka Wachezaji
wa Zanzibar Heroes kutunza afya na kuimarisha mazoezi yao ili michuano ya
mwakani waweze kuwaletea Wazanzibar kikombe cha Ushindi wa Mashindano
hayo.
Ameongeza kuwa kiwango cha
mchezo walichoonesha vijana hao kiliwasisimua Wazanzibari wengi na kuwasababisha
kutenga muda wao kwa ajili ya kuangalia timu yao kila ilipokuwa
ikicheza.
Aidha aliwataka Wachezaji
hao kuitumia fursa ya kuonana na Rais kuelezea mipango wanayodhani itakuwa bora
katika kuimarisha Timu hiyo kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upende wake Meneja wa
Timu ya Zanibar Heroes Salim Msabah ameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kushirikiana bega kwa bega na Chama cha Soka Zanzibar ZFA katika kuhakikisha
timu inapatiwa maandalizi ya mapema ndani na nje ya Nchi ili kuimarisha kikosi
cha timu hiyo.
Amesema anaamini Zanzibar
kuna vipaji vya kutosha katika fani ya Soka na hivyo kinachohitajika ni namna
bora ya kuviendeleza vipaji hiyo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya
mapema.
Nahodha wa Timu hiyo Nadir
Haroub amesema lengo lao lilikuwa kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo lakini nafasi
waliyoipata ya Mshindi wa tatu imewafariji kutokana na kuifunga timu pinzani
kwao.
Amedai kuwa ushindi huo pia
utawajengea heshima wale wachezaji wa Zanzibar wanaocheza Soka katika ligi ya
Bara kutokana na kuifunga Kilimanjaro Stars ambayo wanacheza wake wanacheza wote
katika ligi hiyo.
Timu ya Zanzibar Heroes
iliibuka Mshindi wa Tatu wa Mashindano ya Challenge yaliyofanyika nchini Uganda
baada ya kuichapa Kilimanjaro Stars kwa mikwaju ya Penalti 6-5 na kufanikiwa
kupata zawadi ya kitita cha Dola za Marekani 10,000.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment