WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara),
wamembana mkurugenzi wao, Akashambatwa Lewanika, wakimtaka awalipe
mishahara yao ya miezi mitatu.
Msimamo huo waliufanya jana katika makao makuu ya Tazara jijini Dar es Salaam, baada ya mkurugenzi huo kukutana na wafanyakazi hao ili kutoa ufafanuzi kuhusu kucheleweshwa kwa mishahara yao.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Elasto Kiwele, alisema shughuli za treni zitakaposimama na wateja kuanza kudai fedha zao, itakuwa mbinu sahihi ya kulipwa kwa madai yao.
Alisema kama Serikali na menejimenti ya Tazara haitalipatia ufumbuzi tatizo la kulitulipwa mishahara watatangaza mgomo.
“Safari hii ama watufukuze wafanyakazi wote au watulipe mishahara yetu yote, hiyo ndiyo kauli yetu na hatuogopi vitisho vya kufukuzwa kazi, maana tabia hiyo imekuwapo sana, ila wakitoa mshahara wa mwezi mmoja tunapokea na kuendelea na tafakari yetu,”alisema Kiwele.
Akiunga mkono hoja, mmoja wa wafanyakazi aliyejitambulishwa kuwa ni Musa Joseph alisema njia sahihi ya kupata madai yao ni kusimamisha uendeshaji wa treni inayofanya kazi jijini Dar es Slaam.
“Ili ujumbe wetu umfikie Mwakyembe, naunga mkono kusimamisha safari za treni ya hapa Dar es Salaam. Tukubaliane kwamba kuanzia sasa usafiri huo usimame asitoke mtu hapa kwenda kazini,”alisema Joseph.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Akashambatwa alisema mamlaka itakuwa tayari kulipa mishahara ya Oktoba tu.
No comments:
Post a Comment