tangazo

Sunday, December 30, 2012

DIGITALI KUANZA DAR PEKEE

 
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kununua ving'amuzi vya Startimes eneo la Bamaga jijini Dar es Salaam jana katika siku za mwisho kabla Mamlaka ya Mawasiliano nchini (Tcra) kuhamisha matangazo ya televisheni kutoka mfumo wa Analojia kwenda digitali.Picha na Silvan Kiwale 

WAKATI zimebakia saa 24 Tanzania kuungana na nchi nyingine duniani kuanza kurusha matangazo ya televisheni kwa mfumo wa Dijitali zikiachana na ule wa Analojia, imebainika kuwa mpango huo utaanzia Mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Habari za ndani kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), zilizolifikia Mwananchi Jumapili, zinaeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam pekee, ndiyo litakuwa la kwanza kuingia kwenye mfumo huo kuanzia Januari mosi, 2013 na siyo mikoa mingine nchini.

TCRA, imeshatangaza kuwa itaufunga mfumo wa analojia ifikapo Desemba 31 mwaka huu yaani kesho.

Habari hizo zimeeleza kuwa mamlaka hiyo imeamua kuchukua hatua za tahadhari katika utekelezaji wa mpango huo muhimu, kwa kuanza na mji mmoja baada ya mwingine, ambapo  mwezi mmoja baada ya Dar es Salaam kuanza kutumia mfumo wa dijitali, utafuatia Mkoa wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alipoulizwa aliliambia gazeti hili jana kwamba mamlaka yake itatoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

“Hatuwezi kukurupuka katika suala hili, tuko makini, lakini kesho (leo), tutakuwa na mkutano wa wanahabari kwa ajili ya kueleza mikakati mbalimbali na jinsi tulivyojipanga katika jambo hili,” alisema Profesa Nkoma.

Tayari TCRA imetaja miji mingine mbali ya Dar es Salaam ambayo imeshaunganishwa katika mfumo wa dijitali kuwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Tanga, Mbeya, Moshi na kwa sasa mji wa Morogoro unajengewa miundombinu husika.

Habari zaidi zilieleza kuwa kwa utaratibu uliopo sasa itachukua miezi kadhaa kabla ya kuzimwa kwa mfumo wa analojia katika miji minane ya awali, ambapo pia itachukua muda mrefu zaidi kuzimwa mfumo huo nchi nzima.

Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU), limezitaka nchi zote duniani kuhamia kwenye mfumo huo wa kurusha matangazo ya televisheni wa dijitali kutoka mfumo wa analojia ifikapo Julai 2015.

Ikiwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Tanzania imeanza kutekeleza azimio la nchi hizo ilizozitaka kufanya hivyo mwaka huu wa 2012, badala ya kusubiri hadi tarehe ya mwisho iliyowekwa na ITU.  

Wakati Tanzania ikiwa mstari wa mbele kuhamia kwenye mfumo huo wa dijitali, ingawa kwa mtindo wa awamu, nchi nyingine wanachama wa EAC hasa Kenya na Uganda bado hazijaingia katika mfumo huo.

TCRA imezikabidhi kampuni tatu kufanya kazi ya usambazaji wa mfumo huo wa dijitali, ambazo ni Basic Transmissions  inayoundwa na Kampuni za IPP Media na Sahara

Communications, Kampuni ya Ting ya Agape Associates na Star Media Tanzania Limited (Startimes) ambayo ina ubia na  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Star Communications and Technology ya China.

TCRA imekuwa ikielezea kuwa Tanzania ipo tayari kujiunga na mfumo huo kwa kuwa asilimia kati ya 22 kati ya 24 ya nchi ambayo inatumia analojia, tayari imefikiwa na mtandao wa mfumo wa dijitali, ikijumuisha miji minane ambayo kwa kiasi kikubwa kampuni ya Startimes imeifikia.

Hata hivyo, baadhi ya watu wameshindwa kuzielewa takwimu hizo kwa kuwa mitambo ya analojia ipo katika mikoa kadhaa nchini, ambayo bado haijapata mfumo wa dijitali. Mikoa hiyo ni pamoja na Lindi, Tabora, Bukoba, Musoma, Kigoma na Singida.

Kampuni ya Startimes ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi ambapo hadi sasa inakadiriwa kufikisha wateja 350,000,  Kampuni ya Ting ikiwa na wateja 10,000, huku Kampuni ya Basic Transmissions ikitangaza kuanza
shughuli zake hivi karibuni.

Bei ya king’amuzi ni Sh39,000 ingawa mnunuzi anapaswa kulipia fedha za ziada kwa ajili ya kifurushi atakachochagua.

Hata hivyo, utata bado unagubika urushaji huo wa chaneli za bure ambazo ni ITV, Star TV, TBC1, Channel Ten na Eat Africa TV ikielezwa kuwa wamiliki wa vituo hivyo hawataki zionyeshwe bure kwenye kila king’amuzi bali ving’amuzi vyao pekee.

TCRA imeeleza kuwa kwa sasa imefanikiwa kupata ufumbuzi wa muda, ambapo chaneli zote zinaweza kuonekana bure kwenye kila king’amuzi.

Wananchi wachangamkia ving’amuzi
Katika hatua nyingine, gazeti hili lilifika katika ofisi za makao makuu ya Startimes jijini Dar es Salaam na kukuta mamia ya wananchi wakiwa katika foleni ya kununua ving’amuzi hivyo.

Baadhi ya wananchi hao walionyesha masikitiko yao baada ya kufutwa kwa malipo ya mwezi ya Sh9,000, badala yake kubaki malipo ya Sh23,000 na 36,000 kwa mwezi.“Kwa sasa wametoa ofa, ukinunua king’amuzi kwa Sh39,000 utalipia malipo ya mwezi ya kati ya Sh13,000 au Sh23,000, kile kifurushi cha bei nafuu wamekifuta na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa,” alisema Hadji Jumanne mkazi wa Kijitonyama.

Naye Happy Lazaro alisema Serikali inatakiwa kuongeza muda ili kuwapa fursa wananchi kununua ving’amuzi hivyo kwa kuwa hivi sasa imekuwa vurugu na huenda mitambo ya analojia ikazimwa huku wengi wakiwa hawajapata ving’amuzi hivyo.

Hata hivyo, watendaji wa kampuni hiyo waligoma kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazotolewa na wateja wao ikiwa ni pamoja na ubovu wa baadhi ya ving’amuzi, mabadiliko ya bei ya vufurushi kwa maelezo kuwa siyo wasemaji.

Mwili wa mwanamke aliyebakwa warejeshwa India kwa mazishi

 

NEW DELHI, India

MWILI wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi umerejeshwa nchini humo kwa ndege maalumu ya kukodi.
Balozi  wa  India  nchini  Singapore, T.C.A Raghavan  aliwaambia waandishi wa habari jana, saa  kadhaa baada  ya  mwanamke  huyo kufariki kutokana  na  viungo  vyake  kushindwa kufanya  kazi katika hospitali nchini Singapore  ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu walisafirishwa kwenda India katika ndege maalumu ya  kukodi  mchana wa  jana Jumamosi, kwa mujibu wa Raghavan.

Waziri  Mkuu wa India,  Manmohan Singh alisema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mwanamke  huyo  ambaye alifanyiwa  vitendo  vya  kinyama  kwa kubakwa  na kundi  la  vijana na kwamba  maandamano  yaliyozuka  kutokana na kitendo  hicho “yanaeleweka”.

“Nimesikitishwa  mno  kufahamu  kuwa mwathirika huyo wa mashambulizi ya kinyama yaliyofanyika  Desemba 16 mjini New Delhi ameshindwa kunusurika kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata baada ya shambulio dhidi yake, “ aliandika waziri  huyo mkuu katika tovuti yake.

“Tumeshaona hisia na nguvu ambazo tukio hili limesababisha. Hii ni hali ambayo inaeleweka kutoka  kwa vijana wa India  ambao wanataka mabadiliko ya kweli.

“Nataka  kuwaambia, familia yake na taifa  kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure.”

India imetikiswa na maandamano makubwa tangu msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 aliposhambuliwa kinyama  katika basi mjini New Delhi na kundi la watu sita.

Serikali imekuwa ikijaribu kulituliza wimbi  la hasira kwa  kuahidi adhabu kali kwa uhalifu mkubwa unaohusiana na  ngono pamoja na kuunda tume maalumu ya uchunguzi kuhusiana  na jinsi ya kushughulikia kesi za ubakaji.

Wakati maofisa wakijitayarisha kwa ghasia zaidi mitaani, polisi waliongezwa katika eneo la kati la mji mkuu wa India kabla ya mwili wa msichana huyo kurejeshwa  nchini  humo jana.

Ofisa wa polisi wa mjini New Delhi, alihimiza watu kuomboleza  kifo cha  mwanamke  huyo kwa  amani  wakati  maeneo  kadha  ya  mji  huo mkuu  yamefungwa.

Singh, ambaye  hapo  kabla  alitoa  wito wa  utulivu , alisema kuwa  itakuwa, “Heshima  kubwa  kwa  kumbukumbu  yake  iwapo tutaweza  kuelekeza  hisia zetu hizi  na  nguvu  katika  kuchukua hatua  sahihi. Kwa muda huu tunahitaji mjadala wa maana na uchunguzi kuhusiana na mabadiliko ya lazima  na haraka ambayo yanahitajika katika mtazamo wa jamii.

 “Ni  matumaini  yangu  kuwa  tabaka  lote  la  kisiasa  pamoja  na jamii yote  itatenga maslahi yao  finyu ya binafsi na ajenda  ili kutusaidia  kufikia hatima  ambayo tunaikusudia, na kuifanya  India kuwa mahali bora na salama  kwa wanawake kuweza  kuishi.

UK PAPER TALK ABOUT TRANSFER WINDOW IN JANUARY 2013

Good Morning all football fans! Here Your Sunday's morning paper talk:-

Wesley Sneijder is on his way out of Inter Milan and it could well be Manchester United where he lands as a replacement for Paul Scholes - (THE SUN)

Real Madrid and Paris Saint-Germain are leading the chase to sign Chelsea left-back Ashley Cole, who is out of contract at the end of the season - (SUNDAY MIRROR)

Manchester City's top January prize is a new central defender, with Borussia Dortmund's Mats Hummels and Neven Subotic towards the top of their shoppinglist- (SUNDAY TIMES)

Newcastle midfielder Yohan Cabaye has emerged as a target for Arsenal despite him being out until February with a groin injury -they are hoping to pay much less than the £20m that was quoted last summer - (STAR ON SUNDAY)

Reading hope to add to their midfield in January with a loan deal for Spurs' Tom Huddlestone near the top of their list - (MAIL ON SUNDAY)

Real are also on the trail of Manchester United keeper David de Gea, and willing to pay £22m to install him as a long-term replacement for veteran Iker Casillas - (THE SUN)

Pep Guardiola will spur any advances from Manchester City this summer with his sights set on taking over from Sir Alex Ferguson when he eventually steps aside at Old Trafford - (STAR ON SUNDAY)

The Gunners are also leading the race to sign highly-prized Southampton left-back Luke Shaw,with a fee of £5m expected to get a deal done - (MAIL ON SUNDAY)

Real Betis midfielder Benat, who has been drawing rave reviews inSpain this season, is a January target for Tottenham - (STAR ON SUNDAY)

QPR are yet to agree a pay-off with former manager Mark Hughes and assistants Eddie Niedzwiecki and Mark Bowen, with all three still being paid as part of their cancelled contracts - (SUNDAY MIRROR)

Fulham hope to sign Wolfsburg defender Alexander Madiung to solve their problem with depth at centre-back - (STAR ON SUNDAY)

Liverpool and Newcastle are hot on the trail of France U21 centre-back Nicolas Isimat-Marin, who has impressed for Valenciennes this season and might be availablefor a relatively cheap £3m - (THE SUN)

Blackburn have MK Dons manager Carl Robinson high on their shortlist as a potential replacement for Henning Berg - (SUNDAY MIRROR)

Spurs chairman Daniel Levy has slapped a £60m price tag on Gareth Bale to try and ward off January suitors Real Madrid - (SUNDAY MIRROR)

Arsene Wenger's hopes of signingManchester United winger Nani, who is waiting on a new contract,appear to have been dashed by Sir Alex Ferguson - (STAR ON SUNDAY)

QPR boss Harry Redknapp is bound to be busy in the January transfer market and he is desperate to make Everton defender Sylvain Distin part of his squad - (SUNDAY MIRROR)

Aston Villa defender Richard Dunne could be on his way to the MLS with the New York Red Bulls by the end of January - (STAR ON SUNDAY)

Liverpool, Arsenal and Tottenham are about to go into competition to sign Schalke midfielder Lewis Holtby, who has told the German club he will not be signing a new contract - (SUNDAY MIRROR)

Steve Bruce has emerged as a shock contender in the race for the Blackburn job - (STAR ON SUNDAY)

David Villa is expected to make a move to the Premier League from Barcelona in January, alerting a number of clubs that have recently been linked with the striker - (SUNDAY TIMES)

Arsenal believe they can tempt Everton to sell left-back Leighton Baines for £10m - (STAR ON SUNDAY)

Brighton striker Craig Mackail-Smith is a likely January target for Norwich City - (MAIL ON SUNDAY)

BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAAPILI 30/12/2012 TZ









Mbowe:Ni Dk Slaa 2015

 

CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa atapewa fursa ya kuwania nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza hatua hiyo jana, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mpira, mjini Karatu mkoani Arusha, huku yeye akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa mwenyewe alipoulizwa iwapo ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, alisema: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe?, Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza, nitafikiria kufanya hivyo.”

Katika maelezo yake Mbowe alisema: “Kama Mwenyezi Mungu atampa uhai na afya njema hadi mwaka 2015, Dk Slaa anatosha na Chadema, tutampa fursa nyingine ya kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya urais.”

Huku akishangiliwa na umati wa wana chama wa Chadema Mbowe aliongeza: “Ninataka wanaotumia ugombea Urais kama kete ya kuleta mtafaruku ndani ya Chadema watambue hivyo.”

Alibainisha kuwa, binafsi hana nia ya kuwania urais na badala yake atatumia nguvu, uwezo na kila kilicho ndani ya uwezo wake, kukijenga Chadema ili kushinde uchaguzi na kushika dola.

Mbowe alisema kwa muda mrefu kumekuwapo mbinu na jitihada za kumgombanisha yeye na Dk Slaa kuhusu nafasi ya urais na kutamba kwamba njama hizo kamwe hazitafanikiwa.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alitumia pia mkutano huo kutangaza kumalizika kwa mgogoro uliokuwapo kati ya viongozi wa chama hicho wilayani Karatu.
Hata hivyo, awali katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Mbowe alisema: “

Kikao cha CC (Kamati Kuu), kitakachofanyika Januari mwakani ndicho kitakachoweka utaratibu rasmi wa watu wanaotaka kuwania kiti cha udiwani, ubunge na urais mwaka 2015 na kutangaza nia zao na vigezo vya uteuzi.”

Alisema chama hicho kinakusudia kuwapa nafasi wenye nia kujitokeza mapema, ili kutoa fursa ya kuwaelewa, kuwaandaa, kuwapa mafunzo, kuwaeleza majukumu na wajibu wao, kuwaeleza sera, misimamo na malengo ya chama hicho.

Mbowe alisema kuwa mpango huo utakihakikishia Chadema wagombea wenye uwezo na uhakika wa kushinda mwaka 2015.

“Nia ya mpango huu ni kuepuka watu wanaodandia kuomba uteuzi wa kugombea dakika za mwisho,” alisema Mbowe.

Aliweka wazi kuwa chama hicho kitakuwa makini katika uteuzi wa nafasi ya urais kwa sababu ni nafasi nyeti, isiyohitaji kujaribu wala mzaha.

Alisema kwamba chama hicho hakitasubiri wala kupokea waliokosa fursa za uteuzi katika vyama vingine, kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanaokimbilia Chadema dakika za mwisho akisema kuwa uzoefu umeonyesha wengi wao wanaendelea kuwa mamluki.

Alibainisha kuwa pamoja na vigezo vyote, wagombea hao pia watapimwa kwa uwezo wa kukijenga chama na kujituma, huku akionya kuwa watakaojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote, lazima watambue kuwa mmoja pekee ndiye atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wakati Mbowe akitangaza hatua hiyo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa mwanachama yeyote wa chama hicho kikuu cha upinzani ana uhuru wa kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

Dk Slaa amesema hayo wakati umebakia mwaka mmoja kabla ya taifa kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji huku pia ikisalia miaka miwili kabla ya kufanyika uchaguzi wa mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Kiongozi huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili.

Ingawa awali suala la kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali hasa kiti cha urais ndani ya chama hicho lilizua mgogoro, lakini jana Dk Slaa alisema kuwa mwanachama yeyote anao uhuru wa kufanya hivyo na kwamba hakuna vipengele vya katiba vinavyomzuia.

“Katiba ya Chadema inatoa uhuru kwa mwanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote. Hakuna sehemu yoyote inayoeleza atangaze wakati gani. Hivyo, yuko huru kutangaza nia wakati wowote,” alisema Dk Slaa.

Kauli za Dk Slaa na Mbowe, zimekuja wakati chama hicho kukiwa na msuguano ndani ya chama hicho kuhusu wanachama walioamua kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi kupitia chama hicho.

Pia zimekuja wakati tayari Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche amemtangaza Dk Slaa kuwa ndiye mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Mwaka 2010, Dk Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.

Aidha, tayari Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, naye ametangaza kuwa hakuna kitakachomzuia kuwania urais mwaka 2015 kupitia chama hicho.

Hata hivyo, uamuzi huo wa Zitto, umekuwa ukipata upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama akiwamo Mwasisi ya chama hicho, Mzee Edwin Mtei, ambaye alionya kuwa kitendo cha kiongozi huyo kutangaza mapema nia ya
kuwania urais, kinaweza kukigawa chama hicho.

Kauli ya Dk Slaa kuruhusu wanachama kutangaza nia ya kugombea uongozi kupitia chama hicho, inatafsiriwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni mwarobaini wa mgogoro ambao ungeweza kujitokeza ndani ya chama hicho kama chama kingeendelea kukaa kimya.

Novemba mwaka huu Zitto wakati alikifanya mahojiano na mtandao wa Jamii Forum, alisema kuwa viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

“Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama, maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini watu haohao, wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani.”

Alibainisha kuwa pamoja na vigezo vyote, wagombea hao pia watapimwa kwa uwezo wa kukijenga chama na kujituma, huku akionya kuwa watakaojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote, lazima watambue kuwa mmoja pekee ndiye atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho.

Wakati Mbowe akitangaza hatua hiyo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa mwanachama yeyote wa chama hicho kikuu cha upinzani ana uhuru wa kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

Dk Slaa amesema hayo wakati umebakia mwaka mmoja kabla ya taifa kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji huku pia ikisalia miaka miwili kabla ya kufanyika uchaguzi wa mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Kiongozi huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili.

Ingawa awali suala la kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali hasa kiti cha urais ndani ya chama hicho lilizua mgogoro, lakini jana Dk Slaa alisema kuwa mwanachama yeyote anao uhuru wa kufanya hivyo na kwamba hakuna vipengele vya katiba vinavyomzuia.

“Katiba ya Chadema inatoa uhuru kwa mwanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote. Hakuna sehemu yoyote inayoeleza atangaze wakati gani. Hivyo, yuko huru kutangaza nia wakati wowote,” alisema Dk Slaa.

Kauli za Dk Slaa na Mbowe, zimekuja wakati chama hicho kukiwa na msuguano ndani ya chama hicho kuhusu wanachama walioamua kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi kupitia chama hicho.

Pia zimekuja wakati tayari Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche amemtangaza Dk Slaa kuwa ndiye mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Mwaka 2010, Dk Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.
Aidha, tayari Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye pia ni Naibu

Katibu Mkuu wa chama hicho, naye ametangaza kuwa hakuna kitakachomzuia kuwania urais mwaka 2015 kupitia chama hicho.

Hata hivyo, uamuzi huo wa Zitto, umekuwa ukipata upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama akiwamo Mwasisi ya chama hicho, Mzee Edwin Mtei, ambaye alionya kuwa kitendo cha kiongozi huyo kutangaza mapema nia ya kuwania urais, kinaweza kukigawa chama hicho.

Kauli ya Dk Slaa kuruhusu wanachama kutangaza nia ya kugombea uongozi kupitia chama hicho, inatafsiriwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni mwarobaini wa mgogoro ambao ungeweza kujitokeza ndani ya chama hicho kama chama kingeendelea kukaa kimya.

Novemba mwaka huu Zitto wakati alikifanya mahojiano na mtandao wa Jamii Forum, alisema kuwa viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

“Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama, maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama,” alisema Zitto na kuongeza:

“Lakini watu haohao, wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani.”

KESI YA PEMBE ZA NDOVU UTATA MTUPU KUMBE VIGOGO PIA WAHUSIKA


                                Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema  

WAKATI ujangili unaotishia kutoweka kwa baadhi ya wanyama katika hifadhi za taifa nchini ukiendelea kushika kasi, imebainika kuwa baadhi ya mahakimu, polisi na waendesha mashtaka ni wahusika wakuu wa matokeo ya ujangili ambao ni chimbuko la biashara ya nyara za Serikali zikiwamo pembe za ndovu.
Inakadiriwa kuwa tembo wapatao 30 huuawa kila mwezi na mtandao wa ujangili ambao pia unaundwa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi, ambao wamekuwa wakifanikisha uhalifu huo kwa msaada wa baadhi ya maofisa na askari wa wanyamapori.
Hapa nchini ujangili umekuwa ukifanywa na makundi ya watu wenye silaha haramu katika hifadhi za taifa, mapori ya akiba na maeneo mengine ya wazi, huku kukiwa na taarifa kwamba baadhi ya nyara hasa pembe za ndovu huingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Msumbiji. Wanunuzi wakuu wanadaiwa kuwapo hapa nchini.
Mkurugenzi wa Tanapa, Allan Kijazi anasema hali ni mbaya kwa kuwa taifa linatumia gharama kubwa kuwalinda na kukabiliana na ujangili, lakini wahalifu wanapokamatwa wamekuwa wakiachiwa kinyemela hata pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.
“Ujangili huu ni mtandao mkubwa sana. Wanatumia silaha za kisasa zaidi kuliko hata za kwetu…hata kibali cha kununua silaha hatupati kwa wakati, hali ambayo inadhoofisha jitihada hizi…hapa tulipofikia ushirikiano wa vyombo vyote ni muhimu,” alisema Kijazi.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa, njia kubwa ya kuingizia pembe hizo zipo katika wilaya za Tunduru, Namtumbo na Mbinga mkoani Ruvuma ambako pikipiki hutumika kuvusha kabla ya kusafirishwa kwa kificho hadi Dar es Salaam ambako hupakiwa kwenda nje ya nchi kuuzwa kupitia bandarini.
Kushamiri kwa vitendo vya ujangili kumesababisha kuwapo jitihada za kuukabili, lakini kama alivyosema Kijazi, imebainika kuwa jitihada hizo zinakwazwa na baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola, wakiwamo baadhi ya mahakimu, polisi na waendesha mashtaka.
Uchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa baadhi ya watuhumiwa ambao wamewahi kunaswa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujangili, wametoweka katika njia za kutatanisha na kuacha kesi zikiendelea.
Mchezo mahakamani
Uchunguzi umebaini kuwa, baadhi ya mahakimu wa mahakama za wilaya katika mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga na Kigoma ni sehemu ya mtandao huo, hivyo watuhumiwa wengi wanaokamatwa na nyara, zikiwamo silaha hupewa dhamana na hawarudi mahakamani.
Taarifa za uchunguzi zilizothibitishwa na baadhi ya maofisa wa Tanapa, askari wa wanyamapori na wanasheria wa Serikali zinadai kesi nyingi za nyara licha ya kuwa na uzito, baadhi ya mahakimu walioko chini ya mtandao huo hutoa dhamana kwa masharti nafuu na watuhumiwa huruka dhamana na kuendelea na kazi ya ujangili.
Uchunguzi umebaini mtuhumiwa aliyekamatwa kwa tuhuma za kuwinda faru, nyani na ngiri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mwaka 2010, Madubu Masunga Dusara (33), mkazi wa Ng’walali, haonekani mahakamani baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Shinyanga, Lydia Ilunda kumpa dhamana kwa masharti nafuu.


Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 6 ya mwaka 2010 hakimu alitoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa masharti nafuu bila kuzingatia thamani ya wanyama aliokuwa amedaiwa kuua ambayo ni Sh10.304 milioni.
Kwa mujibu wa sheria, ili mtuhumiwa apewe dhamana anapaswa kuwasilisha fedha taslimu kiasi ambacho ni nusu ya thamani ya wanyama anaotuhumiwa kuwaua au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika, lakini katika kesi hiyo wadhamini hawakuwa wakifahamika na baadaye ilitolewa taarifa kwamba mtuhumiwa haonekani mahakamani.
Kadhalika hakimu huyo alitoa dhamana pia kwa Malango Dusara (42) ambaye ni kaka yake na mtuhumiwa wa awali, Madubu ambaye alikamatwa akiwa na risasi 348, lakini pia akiwa chini ya dhamana taarifa zilifikishwa mahakamani kwamba amefariki dunia.
Hata hivyo, Hakimu Ilunda alisema kuwa chanzo cha kuharibika kwa kesi hizo ni waendesha mashtaka kutopeleka ushahidi kwa wakati.
“Watuhumiwa wanakaa mahabusu miaka bila dhamana wakati wana haki ya kudhaminiwa. Waendesha mashtaka kila wakati wanadai ushahidi haujakamilika na sisi tunatekeleza hitaji la sheria kwa kuwa kupata dhamana kwa makosa kama hayo ni haki ya mshtakiwa,” alisema hakimu huyo.
Alisema tatizo kubwa la waendesha mashtaka wa jamhuri wanasababisha kesi nyingi kufutwa ama washtakiwa kuachiwa huru kwa kuwa hawatoi ushahidi. Hata hivyo, licha ya kudaiwa kwamba amekwishafariki dunia, Malango ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 3 ya 2010 kwa kukutwa na risasi 548, amekamatwa tena na sasa yuko mahabusu.
Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali Mwandamizi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Shinyanga, Hashimu Ngole alilithibitishia Mwananchi kwa simu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
“Alipewa dhamana kwa masharti nafuu na hata sisi hatukushirikishwa, akaruka dhamana …taarifa zikawa zinakuja kuwa amekufa…hilo tulilitegemea maana mwanzoni kabisa tuliitahadharisha mahakama, tukapuuzwa kwa misingi ambayo hatujui…amekamatwa Desemba 14 mwaka huu na sasa yuko mahabusu,” alisema Ngole.
Alisema mdogo wa mtuhumiwa huyo ambaye ana kesi ya kuua faru naye inasemekana yupo hai licha ya mahakama kuarifiwa kwamba alishafariki dunia. Uchunguzi umebaini kwamba kabla ya kudaiwa kwamba wamefariki, tayari mashahidi sita walikuwa wametoa ushahidi wao mahakamani.
Kuhusu kesi zao, Ngole alisema zinaendelea kwa kuwa walijua hawajafa kama ilivyodaiwa kwamba kesi ya mtuhumiwa aliyekamatwa shahidi amebaki mmoja. “Shahidi anatoka Bariadi kuja Shinyanga …amefika mara tatu hakimu hayupo… anarudi kesi ilikuwa Desemba 2 hakimu hakuwapo, imepangwa Desemba 31 mwaka huu sijui kwa tarehe hizo zilizopangwa kama itasikilizwa,”alisema Ngole.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa, hata mawakili wa Serikali Mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wakiendesha kesi hizo hawakuulizwa wakati wa watuhumiwa kupewa dhamana na kama sheria ingezingatiwa, Serikali ingekuwa na uwezo wa kukamata mali za wadhamini baada ya watuhumiwa kuruka dhamana.


“Makosa yao ni makubwa ambayo yanazidi thamani ya Sh10 milioni. Sheria inahitaji dhamana yao walipe nusu ya fedha taslimu na wawe na wadhamini wenye mali isiyohamishika, lakini wao walidhaminiwa na watu wasiofahamika bila hata kutushirikisha sisi, matokeo yake hawaonekani na ujangili unazidi,”alisema na kuongeza:
“Tulichotahadharisha mapema ndicho kimetokea, hii ni hatari watu wameua faru bila hata kuangalia thamani ya mnyama wanapewa dhamana kirahisi namna hiyo?” alihoji.
Alikwenda mbali zaidi na kudai mwaka 2010 waliamua kwenda Meatu kuhakikisha kesi za watuhumiwa wa nyara zinashu ghulikiwa na kuisha, lakini kati ya kesi 80 watuhumiwa wote walikuwa nje ya dhamana na hawaonekani mahakamani.
“Waliokuwa wanafika hawafiki 10 tukalazimika kufuatilia na lugha huwa hiyo kuwa wamekufa…kama hakutafanyika mageuzi katika vyombo vyetu vya uamuzi hata operesheni zingefanyika nyingi hakuna mafanikio…Tanapa wanafanya kazi sana tena katika mazingira magumu, wanaleta watu wanaachiwa tutegemee nini,” alisema.
Hukumu nyingine
Ngole alisema hukumu ambazo zimekuwa zikitolewa zinakatisha tamaa, huku akitoa mfano wa kesi namba 3 ya uhujumu uchumi ya mwaka 2010 ya Masanja Maguzu ambaye alikamatwa akiwa na silaha aina ya SMG, risasi 31 na magazine 3.
Alisema Maguzu kabla ya kukamatwa na silaha hizo alikuwa tayari ametumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuua wanyama ndani ya hifadhi.
“Kimsingi baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano alitolewa, lakini baadaye alikamatwa na silaha ya kivita nyumbani, risasi na magazine lakini alifungwa kifungo cha nje.”
Alisema hata wanapoomba kukata rufaa hawapewi nakala za hukumu na mwenendo wa shauri. ”Inachukua mpaka miaka mitatu watu wanamaliza vifungo vyao hujapata nakala hiyo…kwa madai kuwa vitendea kazi ni shida,”alisema.
Alisema baadhi ya watoa uamuzi wanatumia udhaifu wa sheria kutekeleza matakwa yao na kwamba uamuzi huo unazidi kuligharimu taifa, hivyo aliomba sheria zilizopo zirekebishwe iwe kama ilivyo kwa makosa ya ubakaji adhabu zake zinakuwa kali.
Wasajili Mwanza, Tabora
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Isaya Alphan alipoulizwa kuhusu tuhuma za mahakimu hao alisema hakuna taarifa sahihi na kwamba amekuwa akizisikia kwenye vyombo vya habari.

“Hilo la Shinyanga liko Kanda ya Tabora naomba uwatafute hao,… hili la watuhumiwa walioachiwa katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti mpaka niangalie kwenye faili… kwa sasa siko ofisini niko likizo mpaka Januari,”alisema Alphan kwa simu.Naye Msajili wa Mahakama Kanda ya Tabora, Thomas Simba aliliambia Mwananchi kwa simu kuwa hajapokea taarifa zozote za malalamiko kuhusu suala hilo.
“Haya masuala ya dhamana ni very complicated (yana mkanganyiko) …sijui kwa hilo la hao wa nyara kupewa dhamana kisha hawaonekani mahakamani…kwa kifupi ni kwamba dhamana ni haki ya mshtakiwa kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 15,”alisema Simba na kuongeza:
“Katika ibara ya (1) kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru, (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa uhuru wake isipokuwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria.”
Hata hivyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu masharti ya dhamana kwa watu walioua wanyama wenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni Simba alisema:
“Kwa kuwa hilo liko mahakamani sipendi kulisemea nini kilipaswa kufanyika… kama kuna mambo hayaendi vizuri wahusika wanatakiwa kukata rufaa kuja mahakama ya juu kupinga uamuzi huo.”
Hata hivyo, Mwananchi lilibaini kuwa msajili huyo ni mgeni katika kituo hicho cha kazi kwani amekaa kituoni hapo kwa muda usiozidi miezi minane, akitokea Kanda ya Kigoma alikokuwa akifanya kazi.
Itaendelea kesho Jumapili….

CHADEMA YASEMA:SERIKALI NDIO CHANZO CHA MVUTANO WA GESI


NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema wananchi wa Mtwara na Lindi wana haki ya kuandamana kuhoji jinsi watakavyonufaika na mradi wa gesi.

Naye, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini,
 John Mnyika amesema njia rahisi ya kutatua migogoro ya namna hiyo ni nchi kuwa na sera  ya mfumo wa majimbo.

Desemba 27 mwaka huu maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga uamuzi wa Serikali kusafirishwa gesi kwa njia ya bomba kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa na Zitto jana alisema hoja iliyotolewa na wakazi wa Mtwara ina ukweli ndani yake na inatakiwa kufanyiwa kazi.

“Wananchi hawa hawasemi kwamba gesi na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi, wanataka umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima, mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima, wanataka bandari  ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini, hawasemi mapato yote ya gesi yatumike Mtwara tu” alisema Zitto.

Wakati huo huo, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema kuwa Waziri wa Nishati na Profesa Sospeter Muhongo amepotosha uma katika kauli aliyoitoa hivi karibuni kwamba sera ya Majimbo ambayo ingeweza kulinda maslahi ya wakazi wa Mtwara haitumiki kokote duniani si sahihi.

Alisema kuwa Profesa Muhongo aliiponda tu kwa sababu ni moja ya sera zilizomo ndani ya katiba ya Chadema lakini si ngeni duniani na imeonyesha manufaa mengi kwa nchi zilizoitumia zikiwepo za Bara la Afrika.

“Suala la sera ya majimbo sio geni duniani.
Nchi kadhaa za Afrika zinafuata mfumo huu mathalani Afrika ya Kusini na Ethiopia,” alisema.

Alitaja faida za sera hiyo kuwa ni kujenga uwezo wa kisiasa, uongozi na uwajibikaji.

Alitoa mfano wa hasara za kutotumia sera hiyo kuwa ni nchi nzima
kuendeshwa na ikulu Dar es salaam hata katika mambo ya madogo nay a kawaida kabisa.

Hali hiyo akaielezea kuwa inachochea urasimu na kuchelewesha mipango ya maendeleo kwa sababu tu uamuzi unatoka ngazi ya juu.

Kuhusu faida alisema: “Sera ya majimbo inaelekeza taifa kuwa na viongozi wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika ngazi mbalimbali.

“Hii ina maanisha kwamba kwa muktadha wa sera ya majimbo ofisi na vyeo vya mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, katibu tarafa vitafutwa.”

Saturday, December 29, 2012

Mwenyekiti CCM-Msiyumbe na maneno ya uchochezi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Mathayo Mwangomo, amewataka wananchi wilayani humo kutokukubali maneno ya uchochezi yanayodhoofisha maendeleo na juhudi za Serikali katika kutatua matatizo ya wananchi wake.

Mwangomo alitoa kauli hiyo wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ruiwa wilayani humo.

Alisema kuwa, hivi sasa Chama cha Mapinduzi ambacho kipo madarakani
kinatekeleza sera zake hivyo wananchi hawana sababu za kuendelea kusikiliza maneno ya kubeza maendeleo yanayofanywa na chama hicho.

“Wananchi mnatakiwa kutokubali maneno ya uchochezi yanayotolewa na wanachache ambayo msingi wake ni kudhoofisha maendeleo na juhudi za Serikali katika kutatua matatizo yenu,”alisema Mwangomo.

Alisema kuwa, CCM imefanya mambo mazuri katika jamii ikiwa ni pamoja na kujenga shule za msingi na sekondari za kata, ambazo zimeongeza kiwango cha elimu nchini.

Mbali na kuwaleeza hivyo wananchi hao, Mwenyekiti huyo pia alipokea kero za wananchi wa kata hiyo ya Ruiwa ikiwa ni pamoja na ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh60 milioni zilizochangwa na wananchi hao kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Gwili ambazo zinadaiwa kutafunwa na diwani wa kata hiyo, Alex Mdimilage, anayedaiwa kumtorosha mhasibu wa shule hiyo na kutoroka na fedha za wananchi zaidi ya Sh27milioni na kuiacha shule hiyo ikiwa haina chochote.

Sambamba na hilo wananchi hao pia walilalamikia vitendo vya diwani wao kuwa, amekuwa kikwazo cha maendeleo ya kata hiyo kutokana na uwajibikaji wake mbovu uliopelekea wananchi wengi kukihama chama hicho.

Akijibu tuhuma hizo mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya, Diwani wa kata ya Ruiwa , Alex Mdimilage alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa mambo yote yanayozungumzwa dhidi yake ni chuki za kisiasa na kwamba kwa kipindi chake hiki amesimamia miradi mbalimbali kijijini hapo na kata kwa ujumla.

Mwenyekiti wa CCM huyo alikiri kuwepo kwa viongozi wazembe wilayani humo, hivyo amewataka viongozi wanaohusika na tuhuma hizo kujiengua mapema na hawatasubiri Takukuru na Polisi na kero zote zilizowasilishwa na wananchi atazifanyia kazi.

BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAAMOSI 29/12/2012 TZ
















Friday, December 28, 2012

Lema amsikitikia anayedaiwa kuwa askari JWTZ Monduli

 
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara. 

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema kama angekuwa ndiye mwenye uamuzi ya mwisho ndani ya Chadema, angempokea kwenye chama hicho askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), aliyepiga naye picha kama kitendo hicho kitamfanya afukuzwe kazi.

“Ingawa wanaofaa kutoa kauli kama hizi ni viongozi wakuu kama Mwenyekiti na Katibu wa Taifa kupitia vikao halali vya chama, lakini binafsi, ningekuwa na uwezo, ningempokea mara moja askari huyu kwenye chama kama ishara ya walio tayari kujitoa mhanga kupoteza vyote ikiwemo kazi kwa ajili ya ukombozi wa taifa iwapo atafukuzwa kazi,” alisema Lema.

Hata hivyo, Lema aliyekuwa akizungumza katika mahojiano maalumu akiwa mjini Moshi kwa mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi, alisema kitendo cha JWTZ kuanza kumwandama na pengine kumfukuza kazi askari huyo, kitafumua chuki kubwa kati ya askari wa vyeo vya chini na wenye vyeo vya juu ambao wengi wanaitumikia CCM kwa nafasi zao, ukiwemo ukuu wa mikoa na wilaya.

Alitoa mfano Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Samuel Ndomba ambaye kabla ya kuhamishiwa Makao Makuu ya jeshi alikoshika nyadhifa mbalimbali na hatimaye kuteuliwa kushika nafasi yake ya sasa, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, cheo kilichompa fursa ya kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati ya siasa mkoa wa CCM, Mkoa wa Arusha.

“Askari huyu mdogo akifukuzwa kazi kwa sababu ya picha aliyopiga na sisi, basi itathibitisha double standard (undumila kuwili)  ya utawala katika taifa letu. Huyu kapiga picha na taarifa ya kusakwa inatolewa na JWTZ , lakini wako wengi ambao ni wanajeshi wa vyeo vya juu ambao siyo tu wanapiga picha na viongozi wa chama tawala bali ni wafanyakazi wa CCM kwa nyadhifa zao wakiwa bado wako jeshini,” alisema Lema.

Alisema ujasiri wa mtu huyo anayeamini kuwa kweli ni askari wa JWTZ kujitokeza kupiga naye picha huku akijua anahatarisha kazi yake, ni ushahidi kuwa wapo askari wengi nchini  waliochoshwa na mwenendo wa CCM.

Alisema ukweli huo unathibitishwa na matokeo ya kura katika vituo vilivyokuwa ndani au jirani na vituo vya polisi na kambi za jeshi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo wagombea wa upinzani walipata kura nyingi ikilinganishwa na wale wa CCM.

Lema aliyepiga picha na askari huyo akiwa na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), alitoa changamoto kwa watu wenye mapenzi mema na taifa hili, kufanya utafiti wa maofisa wa juu wa JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wanaotumikia chama tawala kwa siri au kwa uwazi kupitia vyeo na nyadhifa zao.

“Hawa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM ambao tunashuhudia wakirejea jeshini wakitokea kwenye utumishi wa chama lakini hatujawahi kusikia tamko la kutafutwa wala kuchunguzwa na jeshi kwa kushiriki siasa,” alisema Lema

Alisema hata ikitokea kweli askari aliyepiga naye picha akafukuzwa kazi hatajuta kumsababishia madhila hayo bali atajisikia faraja kwa sababu kitendo hicho kitafungua ukurasa mpyae katika harakati za ukombozi kwa watu kuelewa kuwa siyo kila jaribu au makosa ni mkosi, bali ni hatua muhimu katika kufikia mafanikio ya unachokiamini.

Alisema askari huyo atakuwa ameshinda hofu, vitisho na uoga alivyosema ni miongoni mwa dhambi kuu katika maisha ya mwanadamu na kuwataka Watanzania kutoogopa lolote, hata ikibidi kifo wakati wakipigania haki zao kwani hakuna atakayeishi milele kwa kuogopa kufa.

“Ni heri mtu kuishi miaka michache duniani na Jina lake kubaki linaishi kwa haki na wema kuliko kuishi miaka mingi akatoweka kama mzoga” alisema Lema akimkariri Mwana mapinduzi Steve Biko na kuongeza  “Ni dhambi kubwa katika demokrasia kuupuuza ukweli eti kwa sababu anayesema uongo amejifunza kupiga na kuua,”

Lema aliishauri JWTZ kutekeleza ahadi ya kulinda Taifa hata kwa kukemea kwa maneno wizi wa mali na rasilimali za umma zikiwemo fedha na wanyapori wanaotoroshwa kwenda nje kwa msaada wa waliokabidhiwa dhamana ya kuvilinda na kuvitunza kwa faida ya wote.

Msigwa: CCM mnapoteza muda Iringa

 
    MWENYEKITI wa Chadema Mkoa wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa 

 MWENYEKITI wa Chadema Mkoa wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa ameponda mikakati iliyotangazwa na viongozi wa (CCM) wa Mkoa wa Iringa ya kutangaza dhamira ya kurejesha jimbo hilo mikononi mwa chama hicho akisema kitendo hicho si utatuzi wa kero za wakazi wa Mkoa wa Iringa.
Msigwa alihoji ikiwa chama hicho tawala kitafanikiwa kurejesha jimbo lilikuwa likishikiliwa na CCM kwa miaka mingi kabla ya wananchi kuchagua upinzani mwaka 2010 kama ndiyo njia ya utatuzi wa kero za wananchi.

Akizungumza na gazeti hili alisema anashangazwa na mawazo ya viongozi hao wanaofikiria leo kurejesha jimbo badala ya kushugulikia kero za wananchi ambazo alisema zinakwamishwa na utendaji mbovu wa Serikali ya CCM.

“Leo Iringa gunia mmoja la Mahindi Sh80,000, wananchi wa kipato cha chini hawana uwezo wa kununua, yote haya ni matokea ya Serikali ya CCM ya kushindwa kusimamia na kujali wananchi wake, ikiwa watachukua jimbo hili wanataka kusema ndilo litakuwa suluhisho la migogoro na kero za wakazi wa Iringa mjini?,” alihoji Msigwa na kuongeza:

“Hadi sasa ndani ya CCM hakuna mgombea anayeweza kusimama na kupambana na nguvu ya umma katika jimbo hilo na si lazima nipitishwe mimi na chama changu kugombea bali mtu yeyote atakayeteuliwa wananchi watamchagua ili mradi atapitishwa na Chadema” alisema.

Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini alitoa kauli hiyo jana kufuatia viongozi wa CCM wa Mkoa wa Iringa wakiwa ni wa chama na jumuiya zao kueleza mikakati waliyonayo kuwa ni pamoja na kurejesha Jimbo hilo mikononi mwa chama chao.

Padri aliyepigwa risasi Z’bar aikana Polisi

 
           Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Mpendae

PADRI Ambrose Mkenda ambaye alipigwa risasi Jumanne iliyopita, mjini Zanzibar na watu wasiojulikana amekana maelezo yaliyotolewa na polisi yakimtaja kuwa ni Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa, Padri huyo alisema wadhifa wake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchungaji anayeshughulikia masuala yote ya Kanisa Katoliki visiwani humo.

Alisema hakuwa mhasibu wa kanisa hilo kama inavyoelezwa na kwamba taarifa hizo siyo za kweli.Hata hivyo, Padri Mkenda alisema alikuwa akimsaidia mhasibu kwa kipindi cha miezi mitatu.

“Mimi sikuwa mhasibu wa kanisa kama inavyoelezwa na watu. Napinga vikali taarifa hizo kwani mimi nilikuwa namsaidia mhasibu kwa muda tu kwani hakuwapo,” alisema.

Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo mapya ya Padri Mkenda, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohamed alisema asingeweza kuzungumza lolote kwa kuwa alikuwa nje ya kituo chake cha kazi licha ya kuwa na jibu la madai hayo.

“Sasa nipo Dar es Salaam kikazi. Naogopa kuandikwa kwamba nimetoa ufafanuzi juu ya suala uliloniuliza. Japokuwa majibu ninayo, lakini cha msingi ni kwamba jaribu kumtafuta kaimu wangu Haji Hana anaweza kuwapa majibu,” alisema Mohamed.

Alipoulizwa Kamanda Hana alisema inawezekana madai ya Padri Mkenda yakawa ya kweli kwa kuwa baada ya tukio hilo hakuweza kuzungumza lolote na badala yake maelezo yake yalitolewa na wasaidizi wake ambao ndiyo waliosema kwamba alikuwa mhasibu.

“Padri alikuwa akizungumza kwa ishara, hivyo hakuweza kusema chochote. Wasaidizi wake ndiyo wakatoa taarifa hizo kwamba ni mhasibu wa Kanisa.”

Akizungumzia hali yake Padri Mkenda alisema anaendelea vizuri lakini bado ana maumivu makali katika sehemu za mwili wake ikiwa ni pamoja na kichwani.

SMZ yatoa tamko
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema inafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana kwa Padri Mkenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana muda mfupi baada ya kumjulia hali Padri Mkenda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud alisema Serikali inafanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Alisema kwa sasa ni mapema kujua chanzo cha tukio hilo kwani tayari vyombo vinavyohusika ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi Zanzibar na Tanzania Bara vimeshapewa jukumu la kufanya uchunguzi.

“Tukio hili ni kubwa na limetuhuzunisha. Kwa kutambua umuhimu wa watumishi wa dini nchini, Serikali inafanya uchunguzi wa kina ili kutambua chanzo cha tukio hilo haraka,” alisema Aboud na kuongeza:
“Kwa sasa ni vyema tukawaachia madaktari ili wandelee na uchunguzi wa afya yake lakini ifahamike wazi kwamba Serikali ipo makini na pindi wahusika watakapopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.”

 “Nafahamu kwamba watu wanahisia tofauti lakini nataka mfahamu kwamba sisi kama Serikali hatuwezi kusema chochote kuhusiana na tukio hili kwani bado tunafanya uchunguzi ili kuwabaini wahusika.”
Mkuu wa Operesheni Maalumu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (SACP), Simon Siro ambaye pia alimtembelea Padri huyo jana alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kuahidi kwamba wahusika watakamatwa.

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi. Wote waliohusika watakamatwa na kushughulikiwa kwani kitendo hicho siyo cha kibinadamu,” alisema Siro.

Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Jumaa Almasi alisema hali ya Padri Mkenda inaendelea vizuri na kwamba madaktari wanaendelea kumfanyia uchunguzi pamoja na kumpa matibabu.

Tukio la kupigwa risasi kwa padri wa Kanisa hilo ni lapilli baada ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga kumwagiwa tindikali usoni na kifuani na watu wasiojulikana.

BAADA YA KESI YA LEMA KUTOLEWA HUKUMU HATIMAE YAZUKA MAPYA.

 
 MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema 

MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wanasheria hao walisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda, inapingana na sheria.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa Lema, Method Kimomogoro amepinga madai hayo akisema wanaoipinga pengine hawajapata nafasi ya kuliangalia kwa undani suala la haki ya mpiga kura kupinga matokeo mahakamani.

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
Alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi, Katiba ya nchi na Mahakama, vinampa haki mpiga kura kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.

“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
“Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia,” alisema Profesa Shivji.

Chama cha Wanasheria
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutofurahishwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, sababu ya kuwa mpiga kura ni ipi nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

“Mwaka 2002, sheria zote zilifanyiwa marekebisho na baadaye mwaka 2005, Bunge likatunga sheria mpya inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ikafuta ya mwaka 1985. Sheria hiyo na marekebisho yake, ndiyo inayotawala uchaguzi hadi sasa,” alisema.

Alisema hata kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 1985, tayari kulikuwa na uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja ambayo iliamua kuwa mpiga kura ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

 “Uamuzi wa kesi ya Mgonja ulikuja ‘ku-reflect’ (kuakisi) hata kwenye Sheria ya Bunge ya mwaka 1985. Tangu hukumu hiyo ya Mgonja hakuna uamuzi mwingine wa Mahakama ambao umeshautengua huo, ndiyo maana hata wanasheria wanashangaa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani,” alisema.

Alisema kumekuwa na kesi nyingi mahakamani za wapiga kura kupinga matokeo na kwamba nyingine hata yeye amezisimamia na hakuna wakati ambao Mahakama imewahi kusema kuwa hawana haki hiyo.

Alitoa mfano wa kesi iliyofunguliwa na wapiga kura dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu, Phillip Marmo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Alisema kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na wapiga kura hao kushindwa kuweka mahakamani fedha ya amana kwa ajili ya kuiendesha na si kwa sababu hawakuwa na haki.

Akizungumzia hoja ya Mahakama ya Rufani kuwa hapakuwa na ushahidi kama walalamikaji walikuwa wapiga kura, Stolla alisema hilo halikuwa na ulazima kwa kuwa halikuwa jambo lililokuwa likibishaniwa.

“Hata hivyo, kabla ya kuanza kesi Mahakama Kuu, Jaji Mujulizi (Aloyce) aliitisha vithibitisho ili kujiridhisha kama ni wapiga kura,” alisema Stolla na kuongeza:
“Lakini Mahakama ya Rufani wenyewe walianza kutafuta kama liliibuka Mahakama Kuu na licha ya Mahakama Kuu kuonyesha kuwa ilijiridhisha katika hilo, wao wakakosoa kuwa uthibitisho huo ulipaswa uwe sehemu ya mwenendo.”

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.

Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.

Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.

Mugway ashangaa
Wakili Alute Mughway aliyekuwa akiwatetea wajibu rufaa katika rufaa hiyo, alisema Mahakama imeacha jukumu lake la kutafsiri sheria na badala yake ikatunga sheria mpya ambayo inapingana na Sheria ya Bunge na Katiba ya nchi, Ibara ya 26 (2).

Alisema Kifungu cha 111 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Hukumu ya kesi ya Mgonja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinampa haki mpiga kura kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, miongoni mwa watu wanaoweza kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi ni aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura na kwamba tangu wakati huo kifungu hicho hakijawahi kufanyiwa marekebisho.


Wakili wa kujitegemea, Vedasto Audax alikaririwa na gazeti dada la The Citizen akisema: “Swali langu ni kwamba ni lini uamuzi wa kesi ya Mgonja ulionekana kuwa na makosa kisheria? Ni kuanzia leo baada ya Mahakama ya Rufani kutamka kuwa una makosa?”

Wakili wa Lema
Kimomogoro alisema hukumu ya kesi ya Mgonja haijitoleshelezi kwa sababu haikusema ni katika mambo gani mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo mahakamani huku akisema kwa maoni yake, anakuwa na haki pale tu haki zake kama mpiga kura zinapokiukwa.

“Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea,” alisema na kuongeza:

“Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote.”

Alisema mwananchi wa kawaida tu ambaye hajajiandikisha hata kama akimwona mgombea akitoa rushwa hadharani, hana haki ya kufungua kesi mahakamani, lakini alipoulizwa kwa upande wa mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura alisema hakuwa na rejea za sheria kwa kuwa alikuwa Karagwe kwa mapumziko.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kuikubali.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
“Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambapo haki zake hazikukiukwa,” ilisema Mahakama ya Rufani.

Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa masilahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaIi ya mwaka 1995.

Ilisema kesi dhidi ya Lema haikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye masilahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi masilahi ya jamii yote.

Wednesday, December 26, 2012

SERIKALI YASHINDWA KUONDOA BIDHAA BANDIA NCHINI




LICHA ya kueleza kuwa asilimia 20 ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni bandia, Serikali imeshindwa kutekeleza mikakati yake ya kuhakikisha inasafisha bidhaa hizo sokoni.

Desemba 14 mwaka huu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliwaeleza waandishi wa habari kwamba kama hali hiyo itaachwa iendelee itasababisha madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa jumla.

Dk Kigoda aliwataka wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo kuziondoa sokoni haraka kabla Serikali haijaanza kuziondoa kwa nguvu, huku yeye pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Joyce Mapunjo wakishindwa kueleza zoezi hilo litaanza lini.

Alisema uchunguzi umebaini kuwa, kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani, kuna bandari bubu 32, ambazo hutumika kupakua bidhaa hizo bandia.

Lakini jana akizungumza na gazeti hili, Dk Kigoda alisema bado wizara hiyo inapanga mikakati ya kuhakikisha inaondoa bidhaa hizo pamoja na kuwachukulia hatua watakaobainika kuendelea kuziuza.

“Kuna taratibu tunafanya kwanza kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuingia sokoni na kuzitambua bidhaa hizo” alisema Dk Kigoda.

Alipoulizwa haoni kwamba kuchelewa kwa operesheni hiyo ndio kunazidi kuwafanya wafanyabiashara hao kuingiza bidhaa hizo na hasa katika kipindi hiki cha sikukuu alisema, “Nimesema bado kuna taratibu zinafanyika mbona unataka kuharakisha.”

Dk Kigoda pia alisema mchakato wa kuunda bodi mpya ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bado unaendelea kufanywa.

Wiki tatu zilizopita wkaati akifungua kinu cha kuzalisha Cement katika kiwanga cha Twiga nje ya jiji la Dar es Salaam Dk Kigoda aliliambia Mwananchi kwamba bodi hiyo itatangazwa kabla ya Desemba 31 mwaka huu.

Katika maelezo yake ya Desemba 14 alisema kuenea kwa soko la bidhaa bandia nchini kunatokana na bei za bidhaa hizo kuwa ndogo, hivyo kuwavutia wateja wengi.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni matairi ya magari na pikipiki, mafuta ya kupaka, maziwa ya watoto, nyaya za umeme, simu za mkononi na vyakula mbalimbali.

Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, wizara yake inashirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuchunguza bidhaa zinazoingia nchini kabla hazijasambazwa katika soko.

CHADEMA YASEMA KATIBA MPYA SI YA WANANCHI


 Mabere Marando 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kushtukia mchakato wa Katiba Mpya nchini na kubashiri kuwa Katiba hiyo haitakuwa na tija kwani inalenga kuwalinda na kuwanufaisha watawala badala ya wanachi.
Chadema wamedai kuwa pindi kitakaposhika madaraka, chama hicho kitaamua haraka kuisuka upya Katiba hiyo ili iwape nguvu,mamlaka na masilahi wananchi.
Hayo yalisemwa kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ruaha wilayani Kilosa na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando na kufafanua kuwa vifungu vyote vitakavyoondolewa na kuingizwa kwa mizengwe vitaingizwa baada ya chama hicho kushika madaraka.

“Tupo makini na hili wala msihofu, tunajua wanataka iendelee kuwalinda waliopo madarakani ndio maana wanaogopa kuingiza vipengele vinavyowabana hasa kuendeleza ufisadi na kurithshana madaraka,”alisema Marando.
Marando alisema kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho, atahakikisha wananchi wananufaika na matunda ya uhuru kwa kujiandikisha na washiriki kupiga kura maana Chadema imeshinikiza daftari kuanza kurekebishwa upya kuanzia sasa.

“Tunajua kuwa,Katiba hii itachakachuliwa tu, sasa sisi tunawaahidi Watanzania kuwa mtakapotupatia madaraka tutawaandalia katiba inayowapa mamlaka ninyi na kiongozi atabaki kama msimamizi tu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Marando ametangaza rasmi kubeba mzigo wa kesi zinazowakabili waliokuwa viongozi wa Serikali ya kijiji cha Ruaha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wanaendelea kushikiliwa na polisi katika mahabusu ya Kilosa.

Kwa kuanzia alisema, amewasiliana na polisi mkoa na kuelezwa kuwa wanatambua viongozi hao waliondolewa kufuatia mizengwe ya CCM na viongozi wa wilaya kinyume na sheria na kuwa wamekubaliana na polisi mkoa kupitia Mkuu wa Upelele Mkoa (RCO) kuyaagiza majarada ya kesi zote watuhumiwa wote 13 waliokamatwa kijijini hapo na kutoa uamuzi wenye suluhisho la amani.

Alisema baada ya kupunguza kesi za wabunge wa chama hicho, sasa anahamishisa kambi katika kesi zilizopo mkoani Morogoro ili kuwaondoa shaka walionayo wananchi dhidi ya kesi za kusingiziwa za kisiasa na kuahidi kuzishinda zote na kuliaibisha Jeshi la Polisi na washirika wake.

Hata hivyo, Mwanasheria huyo wa Chadema, aliwataka viongozi wa Serikali wilaya na mkoa kuongoza kwa mujibu wa sheria na kuachana na uongozi wa mazoea kwani sasa Chadema hakitawaachia viongozi wanaoongoza kwa lengo la kuwafurahisha mabwana ambao ni chama tawala.

CHADEMA YAIJIA JUU JWTZ



 MBUNGE wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika 

SIKU moja baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutangaza kumsaka mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa amevalia sare za jeshi hilo, chama hicho kimeibuka na kulijia juu jeshi hilo.

Hata hivyo, mbali na kauli hiyo, jeshi hilo limekijibu Chadema likisema kwamba halifanyi siasa na kwamba litaendelea kumsaka mtu huyo, kwa kuwa kanuni zake haziruhusu askari kushabikia siasa.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema chama hicho kimeshangazwa na kasi ya jeshi hilo kuchunguza tukio hilo, huku akidai kwamba kuna masuala mazito ambayo hayajatolewa ufafanuzi kama lile la Meremeta.

“Serikali ilikataa kulifuatilia kwa madai ya kutokuingilia usiri wa jeshi hilo na halikutolewa ufafanuzi wala kufanyiwa uchunguzi mpaka sasa,” alisema Mnyika na kuendelea.

“Isitoshe Septemba, mwaka huu katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Iramba, aliyekuwa Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Mwigulu Nchemba (aliwahi kutoa matamko kuhusu JWTZ), lakini jeshi halikufikiria kuyatolea tamko.”

Mnyika alidai pia kuwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.

“Kauli ile ya Shimbo ni ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM. Mbona jeshi halichunguzi kauli hiyo hata baada ya Shimbo kustaafu?” alihoji Mnyika.

Mnyika alisema kwamba Chadema hakitaki kutumia tukio hilo la askari kuhalalisha makosa mengine, bali inataka sasa JWTZ iwajibike kwa kila jambo linalolihusu badala ya kukimbilia masuala yaliyofanywa na askari wadogo.

Hata hivyo, Mnyika alisema chama hicho hakipo tayari kuingia katika mvutano na jeshi kuhusiana na tukio la askari huyo kujihusisha na siasa mpaka jeshi hilo litakapokamilisha uchunguzi na kutoa taarifa yake kwa umma.

Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema kuwa jeshi litaendelea kujiweka kando na shughuli za siasa na kusisitiza kuwa mtumishi wake yeyote anayetaka kujiingiza kwenye majukwaa ya kisasa anapaswa kujitoa jeshini.

Akijibu hoja za Chadema kuhusiana na tamko lilitolewa na aliyekuwa Mnadhimu wa jeshi hilo Shimbo aliyewataka wanasiasa kutogomea matokeo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Mgawe alisema: “Ebwa ehh! Na wewe sasa unataka kuniingiza kwenye siasa, mimi sitaki kuingia huko, lakini nikueleze kuwa sisi kama wanajeshi tuko royal (utii) kwa Serikali iliyoko madarakani,” alisema Mgawe.

Alisema kwa mujibu wa sheria, Jeshi halipaswi kufungamana na itikadi zozote za kisiasa kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kulitumbukiza taifa kwenye hatari.

 “Leo huyu anaingia kwenye mkutano wa chama na sare za jeshi, kesho atakuja mwingine na silaha, huoni kwamba sasa tutakuwa tunakaribisha hatari ?” alihoji Mgawe.

MAJAMBAZI YAPORA SH 23 MILLION MOSHI


WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bastola, juzi walimvamia mfanyabiashara mmoja wa eneo la Majengo, Mjini Moshi na kumpora fedha taslimu Sh23 milioni.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:00 mchana wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa akipeleka fedha hizo benki.

Habari za kuaminika zinaeleza kuwa mfanyabiashara huyo (jina tunalo) alipofika katika mzunguko wa magari karibu na Shule ya Sekondari ya Majengo, alivamiwa na kuporwa fedha hizo.

Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kabla ya majambazi hao kumpora fedha hizo, walimzuia kwa gari lao aina ya Toyota Noah na kumtishia kwa bastola.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa bado uchunguzi unaendelea.

Kigogo CUF naye alizwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Julius Mtatiro jana alisherehekea Krismasi kwa majonzi baada ya wezi kupasua kioo cha gari lake kwa dawa maalumu kisha kuiba vitu mbalimbali.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Makuburi, Dar es Salaam na mwenyewe aligundua ilipofika asubuhi baada ya kurejea kutoka kanisani.

Katika taarifa yake aliyoiweka kwenye mtandao wa Kijamii wa Facebook, Mtatiro alilielezea tukio hilo kuwa ndiyo Krismasi yake… “Hii ndiyo Krismasi yangu. Kwenda kanisani tu, ndiyo haya yamenikuta. Jamaa wamebeba hadi ‘Dash Board’ ya katikati,” alisema Mtatiro kwenye mtandao huo ambako pia aliweka picha ya gari hilo aina ya Toyota Lexus.

Baadaye Mtatiro alimwambia mwandishi wetu kuwa hajui hasa tukio hilo lilitokea saa ngapi... “Sikuwa najua chochote. Nilipoamka asubuhi nilikwenda kanisani. Mimi nasali katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Makuburi, nilikwenda bila gari kwani siyo mbali ni kama mita 300 tu kutoka nyumbani kwangu.”

“Hata hivyo, wakati naondoka nyumbani niliwaacha vijana wengi tu hivyo sikuwa na wasiwasi wowote. Lakini niliporudi nikakuta wizi huo umeshatendeka.”

Mtatiro alisema wezi hao waliiba vitu hivyo baada ya kuvunja kioo kidogo cha mlango wa nyuma wa gari hilo kwa kutumia dawa maalumu ambayo ilikifanya kiwe chengachenga, kisha kufungua mlango na kuingia ndani ya gari.

Alisema pia waliiba vifaa vya kufungulia vioo (power window) pamoja na redio ya gari hilo… “Vilevile wamepekuapekua ndani ya gari, lakini hawakufanikiwa kupata kitu kingine kwa kuwa sikuwa nimeweka nyaraka zozote muhimu ndani ya gari. Hawakuchukua leseni yangu nimeikuta.”

Mtatiro alisema atatoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.

MWANAFUNZI AKUTWA AMEKUFA NYUMBA YA KULALA WAGENI

MWANAFUNZI  wa kidato  cha tatu katika shule ya Sekondari ya Tongoni nje kidogo ya jiji la  Tanga,  (jina tunalihifadhi) amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe mwanafunzi huyo alikutwa amekufa juzi katika nyumba ya kulala wageni iliyopo barabara ya 21 jijini Tanga.

Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kwamba mwanafunzi huyo aliingia saa 4.00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba.

“Baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye alituuliza kama wameingia mwanafunzi huyo na mwenzake, tulipomwonyesha chumba  walichoingia naye akakodi chumba cha jirani ndipo tukaona wote wakijifungia kwenye chumba kimoja,” alisema mhudumu.

Mhudumu huyo alisema baada ya muda wa saa moja, mvulana na mzee huyo wakaaga kwamba wanatoka huku wakisema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika. Akithibitisha habari hizi, Kamanda Massawe alisema taarifa ya tukio hilo ilitolewa na mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni Jijini Tanga.

“Tatizo ni kwamba nyumba hii ya wageni wahudumu wake hawakuwapa wageni hao daftari ili waorodheshe majina yao hivyo inakuwa vigumu  kuwafahamu,” alisema Kamanda Massawe na kufafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja.

Kamanda Massawe alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.

MISHAHARA YAWA TATIZO KWA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RELI TAZARA

                        
Wafanyakazi wa mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) wakimsikiliza Mkurugenzi wa mamlaka hiyo (hayupo Pichani) kuhusu tatizo la mishahara yao  

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), wamembana mkurugenzi wao, Akashambatwa Lewanika, wakimtaka awalipe mishahara yao ya miezi mitatu.

Msimamo huo waliufanya jana katika makao makuu ya Tazara jijini Dar es Salaam, baada ya mkurugenzi huo kukutana na wafanyakazi hao ili kutoa ufafanuzi kuhusu kucheleweshwa kwa mishahara yao.

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Elasto Kiwele, alisema shughuli za treni zitakaposimama na wateja kuanza kudai fedha zao, itakuwa mbinu sahihi ya kulipwa kwa madai yao.

Alisema kama Serikali na menejimenti ya Tazara haitalipatia ufumbuzi tatizo la kulitulipwa mishahara watatangaza mgomo.

“Safari hii ama watufukuze wafanyakazi wote au watulipe mishahara yetu yote, hiyo ndiyo kauli yetu na hatuogopi vitisho vya kufukuzwa kazi, maana tabia hiyo imekuwapo sana, ila wakitoa mshahara wa mwezi mmoja tunapokea na kuendelea na tafakari yetu,”alisema Kiwele.

Akiunga mkono hoja, mmoja wa wafanyakazi aliyejitambulishwa kuwa ni Musa Joseph alisema njia sahihi ya kupata madai yao ni kusimamisha uendeshaji wa treni inayofanya kazi jijini Dar es Slaam.

“Ili ujumbe wetu umfikie Mwakyembe, naunga mkono kusimamisha safari za treni ya hapa Dar es Salaam. Tukubaliane kwamba kuanzia sasa usafiri huo usimame asitoke mtu hapa kwenda kazini,”alisema Joseph.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Akashambatwa alisema mamlaka itakuwa tayari kulipa mishahara ya Oktoba tu.

Watoto 140 wazaliwa mkesha Krismasi







Wamama wakiwa na watoto wao baada ya kujifungua.  

ZAIDI ya watoto 140 wamezaliwa katika mkesha wa kuamkia Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za wilaya tatu ikiwamo hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa watoto hao ni kutoka katika hospitali ya Temeke ambayo idadi yao ni 53 ambapo wasichana ni 24 wavulana 29 na kati yao pacha ni mmoja.

Kutoka katika hospitali ya Amana wavulana ni 32 na wasichana 30 ni na mmoja wao ni pacha katika hospitali ya Taifa watoto watatu ambao kati yao wawili ni wavulana na msichana mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Daktari wa zamu katika hospitali ya Amana, Pendo Kataponda alisema ni kawaida kupokea wajawazito na
kuwahudumia kipindi cha Krismasi kama ilivyo kwa siku za kawaida.

Kutoka hospitali ya Mwanayamala idadi ya watoto waliozaliwa kwenye mkesha huo ni 25 ambapo kati yao wasichana ni 10 na wavulana ni 15.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliojifungua katika mkesha huo walielezea furaha zao  ambapo walisema wanamshukuru Mungu kwa kuwatunuku zawadi hizo.

Walisema kuwa  hali zao na afya zao watoto wao ni za kuridhisha kitendo ambacho kiliwafanya washindwe kuficha hisia zao za furaha waliyo kuwa nayo.

Mbali na kushukuru walitumia fursa hiyo kupaza sauti zao kuwataka wanawake wenye tabia za kutupa watoto kuacha mara moja kwani wanamuasi Mungu.

Mwasiti Omary mzazi kutoka katika Hospitali ya Temeke alisema kumekuwa na habari nyingi kuhusiana na kutelekezwa kwa watoto ama kutupwa kabisa ni jambo la kulaaniwa.

“Ni bora kama hutaki kuzaa ukatumia kinga au ukaacha kabisa kushiriki tendo la ndoa kuliko kuwatupa watu wasiokuwa na hatia “aliongeza.


Tuesday, December 25, 2012

ZAIDI YA ABIRIA 40 WANUSURIKA KUFA BAADA YA BASI LA KAMPUNI YA NEW FORCE KUGONGANA USO KWA USO NA FUSO MKOANI MBEYA HAPO JANA.

ZAIDI YA ABIRIA 40 WALIOKUWEMO KWENYE BASI LA NEW FORCE WAMEPONA KUFA BAADA YA KUGONGANA NA ROLI AINA YA FUSO MAENEO YA PIPE LINE INYALA  BASI LA NEW FORCE LILIKUWALINATOKEA MBEYA KUELEKEA DSM 

Hili roli aina ya fuso ndilo lililosababisha ajali hiyo kwani lilikuwa lilikuwalinalipita gari lingine bila ya kuangalia kama gari nyingine inashuka mlima na ndipo lilipokutana na basi hilo
Hii ndiyo hali halisi ya ajali hiyo dreva wa fuso kakimbia baada ya kusababisha ajali hiyo
Mtoto Samwelli akisimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwani yeye alikuwa nyuma ya dereva  amesema yeye mkanda ndiyo uliomuokoa kwani mama aliyekuwa jirani yake hakufunga mkanda ameumia vibaya sana 

Badhi ya abilia waliokuwa kwenye basi hilo wakisubiri usafiri mwingine toka katika kampuni ya new force
Baadhi ya mjeruhi hao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu



Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mbeya, Dk. Hamfrey Kiwelu, aliyesimama amesema wamepokea majeruhi 24 na kati ya hao 17 wameruhusiwa baada ya kupata matibabu na majeruhi 7 wamelazwa hospitalini hapo kuendelea na matibabu 

Translate