Kiongozi wa chama cha
upinzani nchini Uganda cha Forum for democratic change –FDC-kanali Kiiza
Besigye, amekamatwa na polisi mjini Kampala kwa kile polisi wanasema ni
kushawishi wananchi kujiunga katika maandamano haramu.
Amekamatwa katika barabara za mjini Kampala
akiwa anatembea kwa miguu huku akifuatiwa na umati wa watu.
Dr Kiiza Besigye amekamatwa na
askari polisi wa kuzuia fujo baada ya purukushani kati ya polisi na
baadhi ya wafuasi wake.Polisi ilikuwa inamvuta kumuingiza katika
karaninga ya polisi huku wafuasi wake wakimvuta kwa nje.
Hata hivyo polisi iliwazidi nguvu na kumuingiza
katika gari lao na kumpeleka kituo cha polisi.
Baadaye naibu msemaji wa polisi Vicent Ssekatte
aliwaambia wandishi habari kuwa Besigye amekamatwa kutokana na hatua ya
kuchochea wananchi
kufanya fujo.
Hatua hii imekuja baada ya Besigye na viongozi
wengine wa upande wa upinzani chini ya vuguvugu la 4GC (For God and My
country) kutangaza mwishoni mwa juma kuanzisha walichoita mchakato wa
matembezi ya uhuru- Walk to freedom kupinga walichoita ufisadi, utawala
mbaya na mengine.
Ilikuwa imepangwa kuanza Jumatatu.
Lakini polisi walikuwa wamepiga marufuku
maandamano na mikutano yote ya hadhara hadi Oktoba 10 baada ya sherehe
za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.
Wengine waliokamatwa ni Meya wa jiji la Kampala
Elias Lukwago ambaye alizuiliwa nyumbani kwake.Lukwago ni mwanachama wa
chama cha upinzani cha Democratic Party DP.
No comments:
Post a Comment