Muungano wa Ulaya umetuzwa tuzo la amani la Nobel mwaka huu kwa juhudi zake za amani barani Ulaya.
Kamati iliyotoa tuzo hiyo, ilisema kuwa Muungano
wa Ulaya umesaidia bara la ulaya kuondokana na vita na kulifanya kuwa
bara la amani.
Tuzo
hiyo inakuja wakati nchi za Ulaya zinakabiliwa na wakati mgumu wa
kiuchumi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 54. We wa
wanachama wa Muungano huo wanakumbwa na mdororo wa uchumi.
Shirika la mwisho kuwahi kupokea tuzo hiyo ni lile la misaada ya matibabu la Medecins Sans Frontieres, mnamo mwaka 1999.
Ikitangaza tuzo hiyo, Rais wa kamati ya Nobel
,Thorbjoern Jagland, aligusia matatizo ya kifedha yanayokumba Muungano
huo, pamoja na vurugu.
Lakini alisema kuwa kamati hiyo inatambua kazi
ya amani, ukereketwa wa demokrasia na haki za binadamu ambayo muungano
huo umejitolea kufanya kwa zaidi ya miongo sitini.
Aidha rais wa kamati hiyo, aligusia juhudi za
muungano huo katika kuleta amani kati ya Ufaransa na Ujerumani katika
miaka baada ya vita vya pili vya dunia.
Alisifu muungano huo kwa kushirikisha Uhispania,Ureno na Ugirriki, baada ya tawala zao za kidekiteta kumalizika miaka ya sabini.
Aliongeza kuwa Muungano huo sasa unaendeleza
kazi ya amani kati ya nchi za Balkan na kusema kuwa sasa Croatia
inakaribia kuwa mwanachama wa Muungano.
Rais wa bunge la Ulaya, Martin Schulz, alielezea furaha yake kwa tuzo hilo.
No comments:
Post a Comment