Majeshi ya Serikali ya Somalia na Umoja
wa Afrika AMISOM yameingia katikati ya mji wa Kismayo siku chache baada
ya wapiganajiwa wa Al Shabaab kuondoka katika mji huo.
Msemaji wa jeshi la Somalia, ameelezea kuwa
mamia ya wanajeshi walihusika katika operesheni hiyo huku majeshi ya
AMISOM yakijiandaa kwa mapambano ya kuutwaa mji huo kutoka mikononi mwa
Al Shabaab.
Wenyeji wa Kismayo wanasema kuwa
wanajeshi wa Kenya waliingia mjini humo kutoka upande wa Magharibi na
sasa wanajiandaa kwa makabiliano ya kuukomboa mji wenyewe.
Kismayo ndiyo ilikuwa ngome ya mwisho ya Al
Shabaab.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuingia
katikati ya mji huo tangu operesheni ya kuwasaka Al Shabaab ilipoanza.
Mji wa Kismayo ni ngome muhimu ya wapiganaji wa
Al Shabaab ambao walikuwa wakiutumia kuwaingizia mapato.
Wakaazi wanasema baada ya kuondoka kwa
wapiganaji wa Al Shabaab hali ya usalama katika mji huo imekuwa sio ya
kuridhisha ambapo kumekuwa na taarifa za baadhi ya viongozi maarufu wa
koo kuawawa.
No comments:
Post a Comment