tangazo

Friday, October 12, 2012

WASHIRIKI WA SHINDANO LA REDD'S MISS TANZANIA 2012 WATEMBELEA SNAKE PARK MESERANI ARUSHA

Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakifurahia kushika nyoka wakati warembo hao walipotembelea eneo la Meserani Snake Park na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, Mamba, Kenge, ndege aina ya  Bundi, Tai na Tumbiri. Warembo hao wapo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii nchini ikiwa ni harakati ya Warembo wa Miss Tanzania kila mwaka kuhamasisha utalii wa ndani. (Picha na Mpigapicha wetu).
----
Redd’s Miss Tanzania kumsaka Top Model leo
Na Mwandishi Wetu, Arusha
 
WAREMBO wanaoshiriki kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania leo usiku wanatarajiwa kupanda jukwaani kumsaka Miss Top Model, katika shindano linalotarajiwa kufanyika hoteli ya Naura Spring, mjini hapa.
Mrembo atakayefanikiwa kutwaa taji hilo moja kwa moja ataingia katika 15 bora ya Redd’s Miss Tanzania, shindano linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
Mpaka sasa Miss Mbulu, Lucy Stephano amejihakikishia kuingia katika hatua hiyo, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Miss Photogenic, lililofanyika Monduli mwishoni mwa wiki.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan Ricco alisema kila kitu kipo tayari n kinachosubiriwa ni kujua nani atatwaa taji hilo.
“Warembo wote wako sawa na wamejiandaa vema kuhakikisha wanatoa upinzani mkubwa, naamini mashabiki watakaohudhuria watapata burudani ya aina yake,” alisema.
Ricco alisema, baada ya shindano hilo warembo wote wanatarajiwa kuondoka mjini hapa kesho asubuhi kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.
Warembo wapatao 30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Translate