ume iliyoteuliwa na serikali ya Afrika Kusini imeanza
uchunguzi wa mauaji ya mwezi Agosti ya watu zaidi ya arobaini katika
mgodi wa madini ya dhahabu nyeupe wa Marikana.
Wengi wa waliouawa walikuwa ni wachimba madini
waliopigwa risasi na polisi wanaoshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi
katika tukio la kwanza kuwahi kutokea tangu kumalizika kwa utawala wa
ubaguzi wa rangi nchini humo.
Tume hiyo imekataa ombi kutoka kwa
familia za wachimba madini zilizotaka uchunguzi huo uakhirishwe kwa muda
wa wiki mbili ikisema kuwa kazi hiyo inahitajika kufanywa haraka
iwezekanavyo.
Uchunguzi huo utaangalia pande zilizohusika na
mauaji hayo, ikiwemo polisi, utawala wa kampuni ya madini, vyama vya
wafanyakazi na serikali.
Pia itawachunguza watu biinafsi au hata makundi
ya watu ikiwa walichochea vurugu zilizosababisha mauaji hayo.
Tume hiyo yenye majaji watatu, ikiongozwa na
jaji mustaafu wa mahakama ya rufaa Ian Farlam, inatarajiwa kuwasilisha
ripoti yake mwezi January mwaka ujao.
Ushahidi wa video
Takriban watu 46 waliuawa katika maandamano ya
wachimba migodi wa Marikana yaliyokumbwa na vurugu na ambayo yalifanyika
kufuatia wiki kadhaa za maandamano
Mauaji hayo yaliyofanyika tarehe 16 mwezi
Agosti, yanasemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kufanyika tangu kumalizika
kwa enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Tume hiyo itaendesha vikao vyake katika ukumbi
wa Rustenburg karibu na eneo walikouawa wachimba migodi hao.
Kuna mipango ya kuweka skrini kubwa sana katika
eneo la Marikana, ili kuwawezesha jamaa za waliouawa kuweza kushuhudia
vikao vya tume hiyo.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg,Milton
Nkosi, anasema kuwa kanda ya video ya kushtua inayoonyesha wachimba
migodi hao wakiuawa, huenda ikatumiwa kama ushahidi dhidi ya polisi.
Wachimba migodi wa Marikana walikubali kurejea
kazini baada ya kukubali nyongeza ya asilimia 22 ya mishahara yao.
Lakini maelfu ya wachimba migodi wengine
wamekataa kurejea kazini katika kile kinachoonekana kama msururu wa
migomo ya migodini kote nchini Afrika Kusini tangu ghasia kukumba migodi
hiyo.
No comments:
Post a Comment