Baadhi ya waislamu wakiwa katika Kituo
cha Polisi cha Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam, ambapo walikwenda kutaka
kumuadhibu mtoto wa kikristo wa miaka 14 aliyekuwa amekojolea kitabu
cha kuran leo.
VURUGU zimezuka leo Mbagala Kizuiani,
Dar es Salaam, baada ya mtoto mmoja mkristo akitaniana na mwenzie wa
kiislamu aliikojolea kitabu cha kurani.
Waislamu wamevamia kituo cha polisi cha
Mbagala, wakitaka mtoto huyo wa kikiristo ili wamuadhibu, lakini polisi
walisimama kidete kutetea hali hiyo.
Baadhi ya waislamu walianza kuchukua
sheria mkononi kwa kuanza kuvunja vyoo vya magari ya polisi yaliyokuwepo
kituoni hapo yakiwemo ya jeshi hilo
Baadhi walianza kuweka magogo na
matofali barabarani kuzunguka kituo hicho cha polisi, ili kuzuia magari
kutoka eneo hilo wa kuingia.
Baada ya muda Kikosi cha Polisi cha
Kuzuia Ghasia kilifika na kuanza kuwatangazia waislamu waliokusanyika
eneo hilo kuondoka mara moja.
Bada ya kuona wankaidi amri hiyo, ndipo
kikosi hicho kikaaamua kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatanya,
wengine kukamatwa na kupelekwa katika vituo vya polisi vya Chang'ombe
na Central.
Makundi mengine ya waislamu wakaamua
kuondoka eneo hilo na kuanza kwenda kuchochea vurugu kwa kuchoma baadhi
ya makanisa eneo la Chamazi kwa madai kwamba wanalipiza kisasi.
Kwa asilimia kubwa vurugu hizo
zimetulizwa na Jeshi la Polisi ambapo pia limetoa amri kwa mtu yeyote
atakayeendeleza vurugu hizo kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
Chanzo ilikuwa hivi
Mtoto wa kiislamu aliyetoka na kitabu
hicho Masjid, alikwenda nacho eneo la uwanja wa mpira alipomkuta mwenzie
mkristo na kuanza kutaniana ambapo alimweleza kuwa ukikifanyia mabaya
kitabu hicho cha dini unaweza kugeuka nyoka au panya.
Ndipo mtoto wa kikikristo mwenye umri wa miaka 14, alibisha na kuamua kukojolea kitabu hicho.
Baada ya kuona kitabu kimekojolewa,
mtoto wa kiislamu aliamua kwenda kumuambia babake juu ya tukio
hilo.Mpaka sasa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi ya la Polisi ambalo
linamuandalia mashitaka kutokana na
No comments:
Post a Comment