Ilikuwa Jumatatu, Machi 12, 1990 wakati
Rais Ali Hassan Mwinyi alipoliita Baraza la Mawaziri na kuwaambiwa
wajiuzulu, akiwemo Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph
Sinde Warioba. Ndipo akamteua Mzee Cigwiyemisi John Samuel Malecela kuwa
Waziri Mkuu ambaye wakati huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza.
Tunajikumbusha tu wajumbe wenzangu.
Wakati huo hakuna mwananchi au chombo cha habari kilichopiga kelele
kushinikiza Rais avunje Baraza hilo, bali ilitokana na utendaji wa
Baraza hilo kutoridhisha. Leo hii eti Rais anasubiri mpaka wanaharakati
au wananchi wapige kelele ndipo aone kuna matatizo? Tujadilini wadau.
No comments:
Post a Comment