tangazo

Tuesday, October 23, 2012

AIBU ISIYO NA MFANO

Na Mwandishi Wetu
WIZI wa aina yoyote ni aibu kwa mtuhumiwa lakini inapotokea staa mkubwa kama Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, kudaiwa kupora vitu kwenye gari, hiyo inakuwa haina mfano.
Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ baada ya kukamatwa.

Kali zaidi ni kwamba Lord anadaiwa kufanya uporaji huo kwenye gari la mwanamuziki mwenzake, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ambalo ni Toyota Rav4, lenye rangi nyeusi.
 
Imedaiwa kuwa Lord akiwa na wenzake wanaojulikana kama ‘wazee wa power window’, waliliotea gari la Ommy na kuiba taa, power window, vioo (side mirrors), redio na vitu vingine kibao.
 
STORI YENYEWE IPO HIVI;
Alhamisi (Oktoba 18, 2012) usiku, Ommy alimuachia gari lake meneja wake anayeitwa Mubenga ambaye alikwenda nalo nyumbani kwake, Kinondoni, nyuma ya Mango Garden, Dar es Salaam.
 
Gari la Ommy Dimpoz baada ya kuibiwa kunyofolewa taa.

LORD ALIVYOHUSIKA
Imedaiwa kuwa baada ya Mubenga kupaki gari hilo nyumbani kwake, Lord akiwa wenzake, waliona ‘dili’ limejipeleka, hivyo wakavizia usiku wa manane watu wakiwa wamelala na kwenda kupora.
 
ALIVYOSHTUKIWA
Kwa mujibu wa Ommy, Ijumaa iliyopita walimkamata mwanamke mmoja ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa mwizi maarufu wa power window na vifaa vingine vya magari kwenye maeneo yote ya Kinondoni.
 
“Yule mwanamke alipobanwa na polisi ndiyo akataja alipo mpenzi wake, akamtaja na Lord Eyez. Kwa kweli inanisikitisha sana kuona msanii mwenzangu anakuwa hivi. Nashindwa nimsaidieje,” alisema Ommy na kuongeza:
 
“Haya mambo yapo polisi na kikubwa ni kwamba Lord ameahidi kutoa ushirikiano wa vitu vyote kupatikana. Wameiba taa za gari, power windows, side mirrors na vitu vingine.”

LORD EYEZ KWELI?
Baada ya kukamatwa Jumamosi iliyopitwa, Lord alipewa mkong’oto na polisi, kama baadhi ya picha zinavyoonesha na aliendelea kushikiliwa mahabusu kwenye Kituo cha Oysterbay, Dar mpaka tulipokwenda mtamboni.
 
Kwa upande mwingine, baadhi ya watu walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba ikiwa Lord atakutwa na hatia basi atakuwa anaponzwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
 
“Unajua Lord sasa hivi anabwia sana. Ni hatari lakini jamaa anasikitisha kwa sababu ni mkali balaa, nakumbuka enzi zile yupo na Ray C (Rehema Chalamila), dah, alikuwa vizuri ila sasa mh!” alisema staa mmoja wa Hip Hop kwa ombi la kutotajwa jina.
 
Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.


KUMBE NA FA ALIIBIWA HAPOHAPO 
Kuibiwa kwa Ommy, kukaibua kisanga kwamba kumbe siku chache kabla, kwenye eneo hilohilo, gari la mwanamuziki, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, aina ya Toyota Mark II GX 110, liliporwa taa, power windows na side mirrors. 

MwanaFA, alisema hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Twitter wakati anampa pole Ommy, Jumamosi iliyopita.

Viongozi wa Uamsho wafikishwa mahakamani Mwanakwerekwe, Wakosa dhamana warudishwa rumande

 Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao

 Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
  Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi
 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kushitakiwa


 Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa Rumande.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Lowasa Mgeni Rasmi VICOBA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala ya Chama chao hicho mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama wa VICOBA Tanzania.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa na ni bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea mpaka jumamosi ijayo Oktoba 27.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akicheza muziki sambamba na Wanachama wa VICOBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Biashara ya Miaka Kumi yam Wajasilia Mali wa VICOBA tangu kuanzishwa kwakwe,iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ikiwa ni ishara ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono Wanachama wa VICOBA wakati wa kuwaaga mara baada ya kufanya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na baadhi ya Wanachama wa VICOBA mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasilia mali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Wanachama wa VICOBA wakijiburudisha kwa kucheza Muziki.
Maandamano ya Wanachama na Wajasiliamali wa VICOBA yakipita Mbele ya Mgeni Rasmi,ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.

MAGAZETI YA LEO JUMAANNE VICHWA VYA HABARI.



 

 

 





 

JK Katika Mkutano Wa UWT Taifa

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakongwe wa UWT katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma  baada ya kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
PICHA NA IKULU

Translate