tangazo

Monday, December 17, 2012

PICHA ZA BAADHI YA MATUKIO YA ONYESHO LA KOFFI OLOMIDE NCHINI TZ 15/12/2012 HUKO LEADERS CLUB

 Mwanamuziki wa Kimataifa, kutoka Congo, Koffi Olomide, akiwaongoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa, wakati wa onyesho lake la Usiku wa Tusker Carnival, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club usiku wa kuamkia leo, ambapo pia alisindikizwa na bendi za Sky Light, Twanga Pepeta, Diamond Sound na Mapacha Wa3.
 Mwanamuziki wa Kimataifa, kutoka Congo, Koffi Olomide na mwanamuziki wake, Cindy, wakiwaongoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa, wakati wa onyesho lake la Usiku wa Tusker Carnival, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club usiku wa kuamkia leo, ambapo pia alisindikizwa na bendi za Sky Light, Twanga Pepeta, Diamond Sound na Mapacha Wa3
 Wanenguaji wa Bendi hiyo, wakishambulia jukwaa....
 Mashambulizi yakiendelea......
 Koffi Olomide, akiimba jukwaani, baada ya kupanda na kushangiliwa na umati mkubwa wa tu waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo, jana usiku kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Hapa ni wakati wanenguaji wa Koffi, akiingia kwenye Jengo waliloandaliwa rasmi kufikia kabla ya kupanda jukwaani, ndani ya Viwanja vya Leaders.
 Koffi, akiwasili katika eneo aliloandaliwa kupumzika kabla ya kupanda jukwaani.
 Koffi, akiteta jambo na Boss wa Tusker, baada ya kuwasili viwanjani hapo.
 Koffi, akinasa picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya SLB watengenezaji wa Bia ya Tusker, iliyoandaa onyesho hilo, kabla ya kuanza kwa Sebene za kupagawisha viwanjani hapo.
 Wanenguaji wa Koffi, akipozi katika picha baada ya kuwasili viwanjani hapo.
 Boss wa Tusker na wafanyakazi wake wakipozi kusubiri kumpokea Koffi.
 Wadau wanahabari nao walikuwepo uwanjani hapo kushuhudia misebene ya Koffi.
 Sehemu ya Mashabiki wa Muziki wa dansi, wakifurahia radha ya muziki wa Koffi.
 Waimbaji wa Bendi ya Sky Ligth, Jonico Frower Maua Gwa, akipozi na wanenguaji wake na mwanamuziki mwenzake, Kushaba.
 Asha Baraka, Macheni na baadhi ya wadau wa muziki wa dansi wakifuatilia onyesho hilo.
 Mshereheshaji wa onyesho hilo, ambaye pia ni mtangazaji wa Tv Ben Kinyaiya, akisebeneka tar tiiiiibu.....
 Hapa sebene la Wana wa Koffi, lilikolea kiasi cha kuwafanya mabosi hawa wa Tusker kushindwa kuvumilia na kuamua kuanza kuyarudi.
 Sehemu ya mapaparazi waliokuwapo kunasa picha za matukio ya onyesho hilo.
 Warembo pia walikuwepo....
 Sehemu ya mashabiki wakifurahia sebene.
 Koffi, akimpongeza Mkurugenzi wa Clouds, Joseph Kusaga, kwa kufanikisha onyesho hilo.
 Huyu ni paparazi wa Ijumaa na Uwazi, akisikitika haikuweza kufahamika mapema alikuwa akisikitika baada ya kukosa tukio gani la picha....

No comments:

Translate