Rais wa China Hu Jintao amefungua rasmi kongamano la
chama tawala ambalo linaanza mfumo mpya wa utawala ambapo watamchagua
kiongozi mara moja katika kipindi cha miaka kumi.
Pia ametoa onyo kali kwa wafisadi akisema kuwa ufisadi bado unaendelea kuwa tatizo kubwa nchini humo
Akihutubia zaidi ya wajumbe 2,000
mjini Beijing, bwana Hu alisema kuwa kukosa kushughulikia tatizo hilo,
huenda kukasababisha pigo kubwa kwa chama.
Aidha Rais Hu anatazamiwa kujiuzulu kutoka
wadhfa wake wa kiongozi wa chama na kumkabidhi Xi Jinping anayeonekana
kuwa kiongozi wa siku za usoni wa Uchina.
China ilipata mafanikio makubwa katika kipindi kilichopita ingawa changamaoto nazo zilikuwa nyingi.
Alitoa wito wa kuwepo malengo makubwa pamoja na kuhimiza bidii.
Hotuba yake ilifungua rasmi mkutano wa wiki moja utakaoshuhudia kuteuliwa kwa viongozi wapya wa chama.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini Beijing, huku
wanaharakati wakiwa wamezuiliwa au kupewa kifungo cha nyumbani,
kulingana na mashirika ya kibinadamu.
Bwana Hu aliwaaambia wajumbe kuwa lazima nchi
hiyo ifuate nyayo za dunia ambayo inabadilika kila kukicha pamoja na
kuzingatia mabadiliko katika mazingira ya nyumbani.
''Lazima tuwe na malengo makubwa, tufanye kazi
kwa bidii na tuendeleze maendeleo ya kisayansi, tuimarishe ushurikiano
na pia maisha ya watu wetu.'' alisema bwana Hu
Mageuzi yatakayofanywa:
Mkutano maalum wa chama cha kikomunsiti kufanyika kila baada ya mwongo mmoja
Viongozi wenye zaidi ya miaka 68 watasataafishwa
Viongozi wapya wakuu kutajwa.
Viongozi hao wameamuliwa lakini bado hawajatajwa.
Mirengo ni muhimu kuliko sera na mfumo wa uteuzi haueleweki
Chanzo cha habari BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment