Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon ameunga
mkono mapendekezo ya Baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuidhinisha
vikosi vya usalama vya kulinda amani vya AU vipelekwe Mali kukabiliana
na wapiganaji wa kiisalamu Kaskazini ya Mali.
Hata hivyo ilikataa kutoa ufadhili wa Umoja wa Matifa katika shughuli hiyo.
Alionya kuwa kuingiliwa kijeshi
katika eneo hilo kutasababisha hatari kubwa za kibinadamu na akataka
kuwe na mipango ya kutuliza hali hiyo.
Wanadiplomasia wanasema kuwa vikosi hivyo
vitatumia nguvu kupita kiasi ilihali vinatakiwa tu kutoa huduma za
kusitisha vita kwa njia ya amani.
Hata hivyo bwana Bana hakutoa msaada wa kifedha
na ksuema kuwa mataifa ya Afrika yanahitaji maswali kuhusu jeshi hilo
litakavyoendesha kazi zake.
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kuungwa
mkono na Umoja wa Mataifa ili kuunda jeshi la pamoja na nchi za Afrika
Magharibi litakalosaidia jeshi la Mali kupambana na waasi.
Jeshi la Mali lilipoteza udhibiti wa Kaskazini mwa nchi ambalo linashikiliwa tena.
Kuhusu mapendekezo yake kwa baraza la usalama la
umoja huo, bwana Ban alisema ataidhinisha wanachama wa muungano wa
Afrika kuunda kikosi cha wanajeshi 3,300 ambao watajulikana kaa AFISMA
kuweza kushika doria nchini humo kwa mwaka mmoja.
Alisema wataisaidia jeshi la Mali kurejesha hali
ya utulivu kaskazini mwa nchi na kupunguza tisho la makundi ya kigaidi
kuvamia eneo hilo
No comments:
Post a Comment