Kiongozi wa baraza linaloandika katiba
mpya ya Misri amesema kuwa pindi tu stakabadhi hiyo itakapokamilika
ikiwa katika hali rasimu, huenda wananchi wakahitajika kushiriki katika
kura ya maamuzi baadaye Alhamisi.
Ikiwa itaidhinishwa na Rais wa Misri Mohamed Mursi, katiba inaelekeza wananchi washiriki katika kura ya maamuzi.
Katika mahojiano na gazeti la Times,
Bwana Musri alipa kuwa atayaachilia mbali mamalka mapya aliyojikabidhi
katiba mpya itakapoanza kutumika.
Taarifa hii inakuja huku mahakama ya kikatiba ikiashiria kuwa itaamua Jumapili ikiwa itavunja baraza hilo
Idara ya mahakama ya Misri iko katika mvutano na
Rais wa nchi hiyo Mohammed Mursi na wafuasi wake wa kiisilamu baada ya
bwana Mursi wiki jana kupitisha sheria inayompa mamlaka kupindukia.
Hofu kuhusu rasimu ya katiba
Hatua hiyo ya rais imezua zogo kote nchini humo.
Huku maandamano yanayopinga hatua ya rais
yaliendelea kote nchini , maafisa katika baraza hilo walisema kuwa
wanakamilisha rasimu ya katiba licha ya bwana Mursi kuliongezea muda ili
kukamilisha rasimu hiyo mwezi Februari.
Kulingana na vyombo vya habari vya serikali, kura ilitarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi kuhusiana na mada hiyo.
Mwandishi wa BBC nchini Misri, Jon Leyne,
anasema kuwa kutolewa kwa katiba katika mazingira haya ya zogo, huenda
ikawa tisho kubwa kwa usalama.
Kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mwenyekiti wa
Jumuiya ya kiarabu,Amr Moussa aliambia waandishi wa habari kuwa ni upuzi
mtupu, na mojawapo ya hatua ambazo hazipaswi kuchukuliwa kabisa
ikizingatiwa hasira ya watu juu ya baraza la kikatiba.
Baraza la kikatiba lina wanachama wengi wa
Muslim Brotherhood na wanasiasa wengine wenye msimamo mkali na ambao
wanamuunga rais Mursi.
No comments:
Post a Comment