Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika bungeni leo akiwasilisha hoja kuhusiana na Uhaba wa Mafuta nchini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (aliyesimama) akijibu hoja ya Mh. John Mnyika.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Ubungo (Chadema) John Mnyika akihoji Kiti cha Spika juu ya serikali kushindwa kuleta bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini Tanzania.
Uhaba
wa mafuta leo umewakimbiza kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma asubuhi,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri
wake George Simbachawene na Steven Masele.
Waziri
huyo na naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa
Ubungo (Chadema) John Mnyika akiitaka serikali itoe sababu ya kutokuja
bungeni leo kutoa tamko la serikali jinsi inavyoshughulikia suala la
uhaba wa mafuta nchini.
Spika
wa Bunge Anne Makinda alimlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusimama
na kujibu hoja ya Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu
hoja yake pamoja na mkakati wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta
nchini.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alilazimika kunyanyuka na kusema kwa ufupi kuwa
serikali ilikuwa ikijiandaa na kuja na hoja nzito ya kueleza umma
mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta nchini.
No comments:
Post a Comment