Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu
cha Dodoma wakiwa kwenye foleni tayari kwa kuchukua majoho yao ambayo
watayavaa katika sherehe za kumalizia safari yao ya miaka mitatu ya
masomo yao ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo Jana na leo
Foleni ikiwa haisogei kabisa huku
wengine wakiendelea kusubiri na wengine kupiga stori mara baada ya
kutokuonana takribani miezi minne tokea walipomaliza masomo yao chuoni
hapo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma
UDOM kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha wakiwa kwenye foleni ya
kuchukua majoho tayari kwa kuhudhuria sherehe za mahafali ya tatu ya
chuo kikuu cha Dodoma yanayotarajia kufanyika tarehe 21 na 22 Novemba
2012 katika viwanja vya Chimwaga
Hapo mwenye nguvu ndie alikuwa wa
kwanza kuingia na mnyonge alisubiri yote hiyo wakigombania kuingia wa
kwanza kwaajili ya kuchukua majoho tu
Huku wengine wakiwa wamejikalia
zao chini wakisubiri vurugu za kuingia kwaajili ya kuchukua majoho
ziishe nao waingie kuchukua majoho yao
Baadhi ya wahitimu mara baada ya
kuchukua majoho yao tayari kwaajili ya sherehe za mahafali ya tatu ya
Chuo Kikuu cha Dodoma yanayotarajiwa kufanyika tarehe 21 na 22 novemba
2012 katika viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo
Mara
Baada ya Kuchukua Majoho yao Wahitimu hawa waliyajaribu kwanza kuona
yanawatosha huku wengine wakisema kuwa "safari hii Majoho Yanatolewa Kwa
GPA likikuenea GPA yako ni kubwa lisipokuenea GPA Yako ni Ndogo"
No comments:
Post a Comment