Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. anatarajiwa kumaliza mkataba wake
mwezi ujao katika klabu ya Simba SC na hadi sasa mustakabali wake haueleweki
kama ataongezewa mkataba au la.
Kumekuwa na
mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji
anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa
kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini
wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa.
Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka
kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Kwa kawaida,
baada ya kumaliza mkataba, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, italazimika
kumpa fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za
Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu
mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana
zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna uwezekano
Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, hasa ikizingatiwa kuwa, kwa sasa hakuna
taarifa zozote za Mzambia huyo kutakiwa na timu, iwe ndani ua nje ya nchi.
Kumalizika
kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa
na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi
ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
No comments:
Post a Comment