tangazo

Monday, September 10, 2012

AIBU; AUNTY LULU ABONDWA AKIGOMBEA PENZI LA PEDESHEE







NI aibu! Mtangazaji ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ anadaiwa kubondwa wakati akigombea penzi la pedeshee maarufu jijini Dar.
 
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Aunty Lulu alichezea kichapo hicho kutoka kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatma, usiku wa Alhamisi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Kundi la Mashauzi Classic lilikuwa likifanya makamuzi.
 
Shuhuda huyo makini aliyeshuhudia mtiti mwanzo hadi mwisho alidai kuwa wawili hao kwa muda mrefu walianza kurushana roho ukumbini hapo huku kila mmoja akimpiga kijembe mwenzake.
 
Alidai kuwa baada ya vita baridi ya maneno, wawili hao walipandwa na hasira ndipo wakavaana na kuanza kupeana kichapo huku Aunty Lulu akizidiwa na makonde hadi walipoamuliwa lakini msanii huyo akawa ameshakula makonde ya kufa mtu.
 
Ijumaa Wikienda lilipofika eneo la tukio lilizungumza na wawili hao kuhusiana na kumgombea pedeshee huyo (jina linahifadhiwa) ambapo kila mmoja alijitapa kuwa mwenzake hana jeuri ya kushea naye mapenzi.

No comments:

Translate