tangazo

Friday, September 7, 2012

Mashambulizi ya kulipiza kisasi Kenya


Ramani ya Kenya

Takriban watu kumi na moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Tana River,Kusini Mashariki mwa Kenya.

Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia watu wakipiga mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha wenyeji kuteketezwa
Eneo hilo ambalo kunaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati ya jamii za Orma na Pokomo.

Watu wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo.

Uvamizi huu umetokea baada ya mashambulizi mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52 kutoka jamii ya Orma wengi wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na kuteketezwa kiasi cha kutotambulika.

Ni katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasia mbaya za kikabila kutokea katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya. Polisi na viongozi wa kijamii walisaidia kutuliza hali na kurejesha usalama kati ya jamii hizo mbili.

Ingawa hali ya wasiwasi ilisalia kukumba eneo hilo.
Jamii hizo mbili za Pokomo na Orma, zimekuwa zikizozana kuhusu matumizi ya ardhi na maji ambazo ni rasilimali adimu.

Wapokomo ni wakulima ambao hukuza chakula kando ya mto Tana wakati jamii ya Orma ni wafugaji wa kuhamahama.

No comments:

Translate