tangazo

Friday, September 14, 2012

HABARI ZILIZO TUFIKIA HIVI PUNDE.

WATU WANANE WAMEKUFA KWA AJALI SINGIDA

WATU tisa wamekufa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha gari la Polisi na Fuso leo mkoani Singida.

Kwa mujibu wa mashuhuda, walisema gari la Polisi lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro kwenda Mara ambapo lilipinduka mara tatu hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na wengine nane kujeruhiwa.

Ajali ya Fuso iliyokuwa imebeba watu na mizigo likielekea mnadani, lilipinduka Mtavila, mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa.

Maiti wa ajali zote mbili zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, ambapo pia majeruhi wanaendelea kutibiwa.
 

No comments:

Translate