tangazo

Thursday, September 20, 2012

MJI WA KISMAYO WAKARIBIA KUTEKWA


Wanajeshi wa Kenya wakipambana na Al-Shabaab
Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir anasema kuwa wanakaribia kuuteka mji wa bandarini wa Kismayo.

Meja Chirchir amekariri kuwa wapiganaji wa Kenya wanaopigania kundi la Al Shabaab ikiwa wataweza kujisalimisha watasamehewa

Kumekuwa na ripoti kuwa wapiganaji wa al-Shabaab wamenza kuutoroka mji huo katika siku chache zilizopita baada ya kuzingirwa na majeshi ya muungano wa Afrika kutoka pande zote

Mji huo ndio ngome ya mwisho ya Al-Shabaab, ambayo huitumia kwa kuingza silaha na zana za kivita kutoka nchi za kigeni.

Muungano wa Afrika unasema kuwa wanajeshi wa Somalia wameuteka mji wa Janaa Cabdlla ngome nyingine ya wapiganaji hao iliyo umbali wa kilomita hamsini Magharibi mwa Kismayo.

No comments:

Translate