tangazo

Friday, September 7, 2012

PICHA ZA WATANZANIA WALIOFARIKI MGODINI LINDI

 

 


 

 WATU saba wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya madini yaliyopo katika kata ya Nandagala wilayani ya Ruangwa mkoani Lindi.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Diwani wa kata hiyo, Andrew Chikongwe alisema kuwa kazi ya kufukua kifusi na kutoa miili ya marehemu hayo ilianza majira ya saa 9 alasiri hadi mapema asubuhi huku wakifanikiwa kupata miili yote.
 
Chikongwe alisema kuwa kazi hiyo ilikuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa zana duni za uokoaji wakati wa kufukua mchanga na hatimaye kupata miili hiyo.
 
Diwani huyo aliwataja marehemu hao kuwa ni Nyang'ana Mkelecha mkazi wa Musoma, Mohamed Omari Fondogoro Mkazi wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa.
 
Wengine ni Rajab maarufu ROGER mkazi wa Musoma, Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo ,Chakoda mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.

No comments:

Translate