tangazo

Monday, September 17, 2012

Mwanamfalme na mkewe kuwasilisha kesi

 
William na mkewe Kate Middleton

 Mawakili wa mwanamfalme wa Uingereza William na mkewe Kate Middleton, wanatarajiwa kuwasilisha kesi katika mahakama moja mjini Paris kubana kuchapishwa tena kwa picha za Kate akiwa nusu uchi.

Wanandoa hao wanataka mahakama kuzuia mauzo ya nakala za jarida la udaku la Closer, ambalo ndilo lilichapisha picha hizo mwanzo.

Picha hizo sasa zimechapishwa na baadhi ya mitandao ya kigeni huku jarida lengine nchini Ireland la Daily Star nalo pia likizichapisha.

Mawakili hao pia wanataka viongozi wa mashtaka nchini Ufaransa kumfungulia mashtaka ya jinai mpiga picha aliyempiga picha Kate akiwa katika likizo ya faragha na mumewe William.

Mwandishi wa BBC mjini Paris , Christian Fraser, anasema kuwa mawakili wengi wanasema kuwa kulingana na sheria kali kuhusu mambo ya faragha nchini Ufaransa, picha hizo zinaonyesha wazi kuwa maisha ya faragha ya Kate yaliingiliwa.

Ikiwa amri ya kisheria itatolewa na mahakama, nakala za jarida hilo zitaondolewa madukani mara moja ingawa hukumu ya mahakama maalum itahusu tu picha hizo nchini Ufaransa.

Hata hivyo hatua hiyo haijazuia kampuni ya Closer nchini Italia yenye kuchapisha jarida liitwalo Chi, kuzuia uchapishaji wa nakala zenye picha ya Kate akiwa nusu uchi.

No comments:

Translate