tangazo

Thursday, September 20, 2012

LIGI KUU VODACOM: Yanga kilio, Simba yachekelea!

MATOKEO:
Septemba 19
JKT Ruvu 0 Simba 2
Mtibwa Sugar 3 Yanga 0
African Lyon v Polisi Morogoro
Ruvu Shootings 2 Mgambo JKT 1
Tanzania Prisons 1 Coastal Union 1
Kagera Sugar 0 JKT Oljoro 0
Toto Africans 2 Azam 2
+++++++++++++++++++++++++++++
VPL_LOGOLigi Kuu Vodacom leo imeendelea kwa Yanga kutandikwa bao 3-0 huko Morogoro mikononi mwa Mtibwa Sugar wakati Jijini Dar es Salaam Mabingwa watetezi  Simba wakiendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa JKT Ruvu bao 2-0.
Huko Morogoro, Mtibwa Sugar walipata ushindi wao wa 3-0 juu ya Yanga kwa bao za Dickson Daudi, Dakika ya 11, na bao mbili za Juma Javu za Dakika za 45 na 77.
Hii ni Mechi ya pili kwa Yanga na hadi sasa hawajaambua ushindi na walitoka sare 0-0 na Tanzania Prisons katika Mechi yao ya kwanza.
Kwa Mabingwa Simba leo ni ushindi wao wa pili kwenye Ligi na bao zao leo zilipachikwa na Amri Kiemba na Haruna Moshi lakini walipata balaa pale Straika wao mkali Emmanuel Okwi alipowashwa Kadi Nyekundu na Refa.
Huko Mwanza, wenyeji Toto African walitoka sare 2-2 na Azam FC huku Toto wakisawazisha bao katika Dakika ya 90 mfungaji akiwa Maganga.
Bao nyingine zilifungwa na Abdulhalim Homoud na Kipre Tchetche kwa Azam na Mussa Saidi kwa Toto.
+++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA Mechi zijazo:
Septemba 22
Yanga v JKT Ruvu    [National Stadium, Dar Es Salaam]
Azam v Mtibwa Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
JKT Oljoro v Polisi Morogoro [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Coastal Union v Toto Africans [Mkwakwani, Tanga]
---------------------------------------------------------------------------------------Septemba 23
Mgambo JKT v Kagera Sugar[Mkwakwani, Tanga]
Simba Ruvu v Shootings [National Stadium, Dar Es Salaam]
African Lyon v Tanzania Prisons [Azam Complex, Dar es Salaam]
+++++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Translate