tangazo

Tuesday, September 11, 2012

Naibu kamanda wa Al Qaeda auawa

Tovuti ramsi ya serikali ya Yemen, imesema kuwa naibu kamanda mkuu wa kundi la kigaidi la al qaeada katika rasi ya Arabia ameuawa.

Tovuti hiyo imesema kuwa jeshi la nchi hiyo limemuua Said Ali Al-shihri, raia wa Saudi Arabia ambaye aliachiliwa huru na Marekani kutoka gereza la Guantanamo Bay mwaka wa 2007.

Hata hivyo kifo cha Al Shihri hakijathibitishwa.

Ripoti zinasema Al shihri ameuawa kusini mwa Yemen ambako majeshi ya serikali yamekuwa yakipambana na wanamgambo wa Kiislamu kwa miezi kadhaa sasa.

No comments:

Translate