tangazo

Wednesday, September 26, 2012

Mbunge kukamatwa kwa uchochezi Kenya

Ghasia za uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007

Mwendesha mkuu wa mashtaka nchini Kenya ameauru kukamatwa kwa mbunge mmoja maarufu nchini humo kwa kuchochea ghasia dhidi ya watu wa kabila moja.

Ferdinand Waititu, ambaye ni naibu waziri wa maji alitoa matamshi ya uchochezi dhidi ya watu kutoka jamii ya Maasai ambao wanaishi katika eneo bunge lake na ambao sana sana hufanya kazi ya ulinzi.

Vurugu lilianza wakati walinzi hao waliposhambulia na kumuua kijana mmoja wa kurandaranda mitaani aliyeshukiwa kwa kitendo cha wizi.
Muda mfupi baada ya bwana Waititu kuwasili katika eneo hilo na kusema '' 

kuanzia leo hatutaki kuwaona watu wa jamii hiyo ( Wamasaai) katika mtaa huu wa Kayole'' vijana hao wa mitaani wakajipanga na kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya mmoja wao.

Mmoja wa walinzi hao aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Hata hivyo mbunge huyo amekana kuwa matamashi yake yalilenga kuwafukuza wamaasai kutoka eneo bunge lake akisema kuwa aliwalenga walinzi wa eneo hilo ambao wengi ni watanzania na ambao pia ni wamasaai.

Aliongeza kuwa matamshi yake ambayo yalirekodiwa hayakukusidiwa. Alisema anakiri kosa lake na hivyo kuomba msamaha.

Wanasiasa wametuhumiwa vikali kwa kuchochea chuki za kikabila huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Zaidi ya watu miamoja wameuwa na maelfu kujeruhiwa katika makabiliano ya kikabila kati ya Waorma na Wapokomo, katika eneo la Tana River.

Uhasama wa kikabila ulisababisha vifo vya maelfu ya watu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007 /2008 kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata

No comments:

Translate