tangazo

Thursday, September 20, 2012

ZIMBABWE INAMSAKA MSHUKIWA WA RWANDA



Dalili za mauaji ya kimbari Rwanda

 Polisi nchini Zimbabwe, wanasema kuwa wameanzisha msako mkali wa afisaa mmoja mkuu wa zamani nchini Rwanda ambaye anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya Kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.

Protais Mpiranya alikuwa kamanda wa ulinzi wa rais mwaka huo na anatuhumiwa kwa kuhusika pakubwa na mauaji ya watutsi 800,000 pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.

Zimbabwe imekuwa ikishutumiwa kwa kumpa hifadhi afisaa huyo wa zamani.
Makama maalum kuhusu mauaji wa kimbari nchini Rwanda imeahidi kumkabidhi zawadi ya dola milioni tano yeyote mwenye taarifa kumhusu Protais.

"Tunamtaka. Awe hai au akiwa amekufa. Tunatafuta taarifa kumhusu ili tumkamate.Hatufahamu mda ambao amekuwa akiishi hapa nchini'' alisema afisaa mkuu wa polisi Zimbabwe Peter Magwenzi.

Mwaka jana afisaa mmoja wa nchi hiyo alikana kuwa Zimbabwe inamhifadhi Protais.

No comments:

Translate