tangazo

Friday, September 7, 2012

Dk Shein amkarib isha Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya watu wa China Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Hui Liangyu baada mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana,akiwa katika ziara ya siku mbili. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Hui Liangyu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa katika ziara ya siku mbili ,Makamo Waziri Mkuu Liangyu akiwa na ujumbe wake walifanya mazungumzo na Rais [Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkaribisha Makamo Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Watu wa China  Mhe,Hui Liangyu,mara alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar jana. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 
NA Rajab Mkasaba , Ikulu
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Hui Liangyu huku China ikiahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo.
 
Katika mazungumzo hayo viongozi hao walieleza ni kwa namna gani nchi mbili hizo zimeweza kukuza na kuimarisha uhusiano huo wa muda mrefu ambao umeweza kuleta manufaa zaidi.
 
Aidha, Dk. Shein alimueleza Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa Zanzibar inajivunia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na China ambao ulianzishwa na viongozi waasisi akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na  Mwenyekiti Mao Tse Dung.
 

No comments:

Translate