tangazo

Tuesday, October 23, 2012

AIBU ISIYO NA MFANO

Na Mwandishi Wetu
WIZI wa aina yoyote ni aibu kwa mtuhumiwa lakini inapotokea staa mkubwa kama Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, kudaiwa kupora vitu kwenye gari, hiyo inakuwa haina mfano.
Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ baada ya kukamatwa.

Kali zaidi ni kwamba Lord anadaiwa kufanya uporaji huo kwenye gari la mwanamuziki mwenzake, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ambalo ni Toyota Rav4, lenye rangi nyeusi.
 
Imedaiwa kuwa Lord akiwa na wenzake wanaojulikana kama ‘wazee wa power window’, waliliotea gari la Ommy na kuiba taa, power window, vioo (side mirrors), redio na vitu vingine kibao.
 
STORI YENYEWE IPO HIVI;
Alhamisi (Oktoba 18, 2012) usiku, Ommy alimuachia gari lake meneja wake anayeitwa Mubenga ambaye alikwenda nalo nyumbani kwake, Kinondoni, nyuma ya Mango Garden, Dar es Salaam.
 
Gari la Ommy Dimpoz baada ya kuibiwa kunyofolewa taa.

LORD ALIVYOHUSIKA
Imedaiwa kuwa baada ya Mubenga kupaki gari hilo nyumbani kwake, Lord akiwa wenzake, waliona ‘dili’ limejipeleka, hivyo wakavizia usiku wa manane watu wakiwa wamelala na kwenda kupora.
 
ALIVYOSHTUKIWA
Kwa mujibu wa Ommy, Ijumaa iliyopita walimkamata mwanamke mmoja ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa mwizi maarufu wa power window na vifaa vingine vya magari kwenye maeneo yote ya Kinondoni.
 
“Yule mwanamke alipobanwa na polisi ndiyo akataja alipo mpenzi wake, akamtaja na Lord Eyez. Kwa kweli inanisikitisha sana kuona msanii mwenzangu anakuwa hivi. Nashindwa nimsaidieje,” alisema Ommy na kuongeza:
 
“Haya mambo yapo polisi na kikubwa ni kwamba Lord ameahidi kutoa ushirikiano wa vitu vyote kupatikana. Wameiba taa za gari, power windows, side mirrors na vitu vingine.”

LORD EYEZ KWELI?
Baada ya kukamatwa Jumamosi iliyopitwa, Lord alipewa mkong’oto na polisi, kama baadhi ya picha zinavyoonesha na aliendelea kushikiliwa mahabusu kwenye Kituo cha Oysterbay, Dar mpaka tulipokwenda mtamboni.
 
Kwa upande mwingine, baadhi ya watu walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba ikiwa Lord atakutwa na hatia basi atakuwa anaponzwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
 
“Unajua Lord sasa hivi anabwia sana. Ni hatari lakini jamaa anasikitisha kwa sababu ni mkali balaa, nakumbuka enzi zile yupo na Ray C (Rehema Chalamila), dah, alikuwa vizuri ila sasa mh!” alisema staa mmoja wa Hip Hop kwa ombi la kutotajwa jina.
 
Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.


KUMBE NA FA ALIIBIWA HAPOHAPO 
Kuibiwa kwa Ommy, kukaibua kisanga kwamba kumbe siku chache kabla, kwenye eneo hilohilo, gari la mwanamuziki, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, aina ya Toyota Mark II GX 110, liliporwa taa, power windows na side mirrors. 

MwanaFA, alisema hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Twitter wakati anampa pole Ommy, Jumamosi iliyopita.

No comments:

Translate