tangazo

Friday, October 12, 2012

FFU YAFYATUA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAISLAMU WALIOKUWA WAMEVAMIA KITUO CHA POLISI MBAGALA KUATAKA KUMUADHIBU MTOTO WA KIKRISTO ALIYEIKOJOLEA QURAN

 Baadhi ya waislamu wakiwa katika Kituo cha Polisi cha Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam, ambapo walikwenda kutaka kumuadhibu mtoto wa kikristo wa miaka 14 aliyekuwa amekojolea kitabu cha kuran leo.

VURUGU zimezuka leo Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam, baada ya mtoto mmoja mkristo akitaniana na mwenzie wa kiislamu aliikojolea kitabu cha kurani.

Waislamu wamevamia kituo cha polisi cha Mbagala, wakitaka mtoto huyo wa kikiristo ili wamuadhibu, lakini polisi walisimama kidete kutetea hali hiyo.

Baadhi ya waislamu walianza kuchukua sheria mkononi kwa kuanza kuvunja vyoo vya magari ya polisi yaliyokuwepo kituoni hapo yakiwemo ya jeshi hilo

Baadhi walianza kuweka magogo na matofali barabarani kuzunguka kituo hicho cha polisi, ili kuzuia magari kutoka eneo hilo wa kuingia.

Baada ya muda Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Ghasia kilifika na kuanza kuwatangazia waislamu waliokusanyika eneo hilo kuondoka mara moja.

Bada ya kuona wankaidi amri hiyo, ndipo kikosi hicho kikaaamua kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatanya, wengine kukamatwa na kupelekwa katika vituo vya polisi vya Chang'ombe na Central.

Makundi mengine ya waislamu wakaamua kuondoka eneo hilo na kuanza kwenda kuchochea vurugu kwa kuchoma baadhi ya makanisa eneo la Chamazi kwa  madai kwamba wanalipiza kisasi.

Kwa asilimia kubwa vurugu hizo zimetulizwa na Jeshi la Polisi ambapo pia limetoa amri kwa mtu yeyote atakayeendeleza vurugu hizo kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Chanzo ilikuwa hivi
Mtoto wa kiislamu aliyetoka na kitabu hicho Masjid, alikwenda nacho eneo la uwanja wa mpira alipomkuta mwenzie mkristo na kuanza kutaniana ambapo alimweleza kuwa ukikifanyia mabaya kitabu hicho cha dini unaweza kugeuka nyoka au panya.

Ndipo mtoto wa kikikristo mwenye umri wa miaka 14, alibisha na kuamua kukojolea kitabu hicho.

Baada ya kuona kitabu kimekojolewa, mtoto wa kiislamu aliamua kwenda kumuambia babake juu ya tukio hilo.Mpaka sasa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi ya la Polisi ambalo linamuandalia mashitaka kutokana na

No comments:

Translate