tangazo

Friday, October 12, 2012

Muungano wa Ulaya wapokea tuzo ya Nobel

Muungano wa Ulaya watuzwa Nobel

Muungano wa Ulaya umetuzwa tuzo la amani la Nobel mwaka huu kwa juhudi zake za amani barani Ulaya.

Kamati iliyotoa tuzo hiyo, ilisema kuwa Muungano wa Ulaya umesaidia bara la ulaya kuondokana na vita na kulifanya kuwa bara la amani.

Tuzo hiyo inakuja wakati nchi za Ulaya zinakabiliwa na wakati mgumu wa kiuchumi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 54. We wa wanachama wa Muungano huo wanakumbwa na mdororo wa uchumi.

Shirika la mwisho kuwahi kupokea tuzo hiyo ni lile la misaada ya matibabu la Medecins Sans Frontieres, mnamo mwaka 1999.

Ikitangaza tuzo hiyo, Rais wa kamati ya Nobel ,Thorbjoern Jagland, aligusia matatizo ya kifedha yanayokumba Muungano huo, pamoja na vurugu.

Lakini alisema kuwa kamati hiyo inatambua kazi ya amani, ukereketwa wa demokrasia na haki za binadamu ambayo muungano huo umejitolea kufanya kwa zaidi ya miongo sitini.

Aidha rais wa kamati hiyo, aligusia juhudi za muungano huo katika kuleta amani kati ya Ufaransa na Ujerumani katika miaka baada ya vita vya pili vya dunia.

Alisifu muungano huo kwa kushirikisha Uhispania,Ureno na Ugirriki, baada ya tawala zao za kidekiteta kumalizika miaka ya sabini.

Aliongeza kuwa Muungano huo sasa unaendeleza kazi ya amani kati ya nchi za Balkan na kusema kuwa sasa Croatia inakaribia kuwa mwanachama wa Muungano.

Rais wa bunge la Ulaya, Martin Schulz, alielezea furaha yake kwa tuzo hilo.

No comments:

Translate