tangazo

Tuesday, October 2, 2012

MAJESHI YAINGIA KATIKATI MWA KISMAYO

Mji wa Kismayo

Majeshi ya Serikali ya Somalia na Umoja wa Afrika AMISOM yameingia katikati ya mji wa Kismayo siku chache baada ya wapiganajiwa wa Al Shabaab kuondoka katika mji huo.

Msemaji wa jeshi la Somalia, ameelezea kuwa mamia ya wanajeshi walihusika katika operesheni hiyo huku majeshi ya AMISOM yakijiandaa kwa mapambano ya kuutwaa mji huo kutoka mikononi mwa Al Shabaab.

Wenyeji wa Kismayo wanasema kuwa wanajeshi wa Kenya waliingia mjini humo kutoka upande wa Magharibi na sasa wanajiandaa kwa makabiliano ya kuukomboa mji wenyewe.

Kismayo ndiyo ilikuwa ngome ya mwisho ya Al Shabaab.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuingia katikati ya mji huo tangu operesheni ya kuwasaka Al Shabaab ilipoanza.
Ramani ya Kismayo

Mji wa Kismayo ni ngome muhimu ya wapiganaji wa Al Shabaab ambao walikuwa wakiutumia kuwaingizia mapato.

Wakaazi wanasema baada ya kuondoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab hali ya usalama katika mji huo imekuwa sio ya kuridhisha ambapo kumekuwa na taarifa za baadhi ya viongozi maarufu wa koo kuawawa.

No comments:

Translate