tangazo

Tuesday, October 9, 2012

Jeshi la Nigeria matatani kwa mauaji


Eneo la Maiduguri
Takriban watu 30 wameuawa na wanajeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mabomu kulipuka mjini Maiduguri. Wenyeji wa mji huo wameelezea ambavyo wanajeshi waliwapiga risasi raia kiholela na kisha kuteteketeza nyumba zao.

Mwenyeji mmoja mjini humo, alielezea kuona kwa uchache kabisa mili tano. Mwandishi mmoja wa habari, wa shirika la AP alisema aliweza kuhesabu takriban miili thelathini.

Taarifa kutoka mjini humo zinasema kuwa wanajeshi waliwafyatulia risasi watu muda mfupi baada ya bomu moja kulipuka katika kituo cha kijeshi.

Wenyeji wanasema kuwa wanajeshi waliwachapa watu kabla ya kuteketeza moto nyumba na maduka. Aidha msemamji wa jeshi alipuuzilia mbali madai hayo akisema hakuwa na ripoti zozote za raia kuuawa.

Wadadisi wanasema kuwa katika mgogoro huu kati ya jeshi na Boko Haram, raia wamekuwa ndio wenye kuumia zaidi. Kwa kuwa hakuna wa kuwaamini kati ya polisi na Boko Haram, wenyeji wanasalia wamenaswa katikati ya mgogoro huu.

Shirika la Huma Rights Watch hivi karibuni lilitoa wito wa polisi wanaowafanyia ukatili watu kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Translate