tangazo

Thursday, September 6, 2012

BASI LAPINDUKA NA KUUA MMOJA MKOANI TABORA.


Na:Robert Kakwesi,Tabora


 Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani uyui.
 

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Tabora,Anthony Ruta,Mrakibu mwandamizi wa polisi,John Kauga,amesema
 ajali hiyo imetokea eneo la kizengi wilayani uyui baada ya basi la kampuni ya Muro kupinduka.

Kauga amesema mwanamke mmoja amefariki duniua katika ajali hiyo ambaye bado    hajatambulika na mwili wake umehifadhiwa 
 chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa,kitete.

majeruhi zaidi ya kumi wamelazwa katika Hospitali hiyo huku Daktari wa Mkoa,Leslie Mhina,akisema majeruhi wanazidfi kuongezeka.

akizungumzia chanzo cha ajali hiyo,mrakibu mwandamizi Kauga amesema ni baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 904 BWA
,Sihaba Mohamed kumuachia utingo wake ambaye jina lake halijapatikana kuendesha basi hilo na kusababisha ajali.

Amesema dereva na utingo wake wote wamekimbia baada ya ajali iliyotokea jana usiku jumanne majira ya saa tatu kasorobo na wanatafutwa.

No comments:

Translate