tangazo

Thursday, July 19, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA AJALI YA MV SKAGIT.

 Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya Boti akiwa na simazi ya kuondokewa na jamaa yake katika  tukio la ajali hiyo, baada ya kuitambua maiti ya jamaa yake iliopelekwa katika viwanja vya maisara.
Wananchi wakiwa katika Ufukwe wa bahari ya Kizingo wakiangalia  kama kutakuwa na miili kuangukia katika ufukwe huo ili kuwatambua jamaa zao.
Wananchi  wakikagua maiti ili kutambua maiti za jamaa zao katika viwanja vya maisara ambavyo vimetengwa kwa ajili kufikisha maiti wanaookolewa katika ajali hiyo.
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wakitowa huduma ya maji na biskuti kwa Wananchi wanaofika kutambua miili ya jamaa zao na watoa huduma katika kituo hicho.

Waheshimiwa Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mashehe wakiwa katika viwanja vya maisara kuwafariji jamaana ndugu waliofiwa na jamaa zao.


Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika viwanja vya maisara kulikotengwa kwa ajili ya kuwatambua marehemu wa ajali ya boti iliotokea jana 18-7-2012 katika bahari ya Zanzibar maeneo ya Chumbe,
Mmoja wa Abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Tatu Piela , akipata  kikombe cha uji kutoka kwa wasamaria waliofika katika viwanja vya maisara , ambaye na mweji wa Isaka Shinyanga, amepoteza  mtoto Said Jumanne mwenye umri wa miezi 9 wake, akisubiri kukabidhiwa maiyi yake kwa ajili ya kwenda kuzika. 

Jamaa  wa Marehemu Sauda Juma ambaye ni Raia wa Ruwanda ambaye ambaye amafariki katika ajali hiyo, wakisubiri maiti yao ili kwenda kuzikwa.


Rais Mstaaf  Mhe Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika eneo hilo maalum kwa ajili ya kuwatambua maiti wa ajali ya boti.


                 










No comments:

Translate