tangazo

Tuesday, July 17, 2012

Mihadarati na Silaha zachochea vita Afrika

                                                                    Ansar Dine

Ongezeko la biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na silaha zilizotapakaa hovyo kwa sababu ya biashara haramu ya silaha, ndio chanzo kikubwa cha machafuko barani Afrika.

Hii ndio kauli aliyotoa rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf.

Katika mahojiano na BBC Bi Sirleaf alisema kuwa kuongezeka kwa makundi kama Boko Haram nchini Nigeria na al-Shabab nchini Somalia ni hali ya kutia wasiwasi.

Pia aligusia uvamizi uliofanywa hivi karibuni na kundi la Ansar Dine nchini Mali.

Rais huyo aliongeza kuwa Liberia itajitolea kuongoza kampeini itakayolenga kupambana na hali hiyo.
Bi Sirleaf amesesma atazishawishi nchi zinazotengeza silaha kutia saini mkataba utakaozuia kusambaa kwa silaha haramu.

Rais Sirleaf aliyasema hayo huku mkutano wa muungano wa Afrika ukiendelea katika mji mkuu wa Ethiopia ,Addis Ababa.

Viongozi wanaohudhuria mkutano huo walitoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuingilia kati mzozo unaoendelea nchini Mali.

Wapiganaji wa Tuareg pamoja na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Ansar Dine walichukua udhibiti wa Kaskazini mwa Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali miezi kadhaa iliyopita .

Jeshi lilichukua madaraka nchini Mali mwezi Machi baada ya kuituhumu serikali kutofanya vya kutosha kusitisha harakati za kamundi ya wapiganaji wa kiisilamu.

Lakini waasi hao walitumia fursa ya mapinduzi kuteka eneo zima la kaskazini mwa Mali, ambalo ukubwa wake ni sawa na Ufaransa.

No comments:

Translate