tangazo

Wednesday, July 18, 2012

Yanga wawachapa 7 Wau Salaam Kombe la kagame.


Mabingwa watetezi wamichuano ya Klabu bingwa Africa Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) Dar Young African 'Yanga' wameishushia kichapo wagen Wau Salaam toka taifa geni la Sudan Kusini goli 7-1 hii leo.

Yanga waliutawala mchezo huo na walikuwa na uwezo wa kuondoka na ushindi wa zaidi ya magoli 12 kama wachezaji wake wangekuwa makini pale walipo sogelea lango la Wau Salaam, ambayo ndio timu iliyofungwa magoli mengi mpaka sasa.

Yanga walianza kuhesabu goli la Kwanza katika dakika ya 12 kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Said Bahamuzi kabla ya kurejea tena nyavuni katika dakika ya 17. Dakika moja mbele Hamisi Kiiza aliipatia yanga goli la 3.


Kiiza alirejea tena kwenye nyavu za Wau Salaam kaitaka dakika ya 25 na 35 akifunga goli la 4 na la 6, huku la 5 likifungwa na Stephane Mwasika katika dakika ya 30 na Yanga kwenda mapumziko wakiwa na hazina ya magoli 6-0.

Kipindi cha pili Yanga kilipoteza nafasi lukuki kupitia kwa Nizar Khalfan, Hamisi Kiiza na Hussein Bahamuzi, wakati Yanga wakiwapumzisha Kelvin Yondan, Mwasika na Haruna Niyonzima nafasi zao zikachukuliwa na Kijiko. Gumbo na Iddrisa Rashidi.

Kalamu ya magoli kwa yanga ilihitimishwa na Nizar Khalfan katika dakika ya 74 kabla ya Wau Salaam kuandika goli la kwanza katika michuano ya Kagame katika dakika ya 90 na mpira kwisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa gaoli 7-1.

Kibaguzi cha mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa ni namna ya goli la Hamisi Kiiza alivyo lifunga katika dakika ya 35, na ndilo linaonekana kuwa goli la mashindano akifunga kwa kisigino, akiunga krosi fupi ya Mwasika.


Katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Taifa ulishuhudia APR wakitoka sare ya bila kufungana na Atletico ya Burundi. Hivyo kundi hilo la A kuendelea kuongozwa na APR wenye point 4 wakufuatiwa na Atletico wakiwa na point 4 kisha Yanga na point zao 3, Wau Salaam wakishika mkia.

No comments:

Translate