tangazo

Wednesday, July 18, 2012

CHEGGE APATA AJALI SEHEMU ALIPOFIA MAFISANGO

                                                Gari La Chegge ambalo amepata nalo ajali


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Said Nassoro ‘Chege’ amenusurika kifo baada ya kutokea ajali ya gari aina ya Corona alilokuwa akiendesha, kumgonga mwendesha pikipiki katika barabara ya Mbozi, Temeke jijini Dar es Salaam, juzi usiku.
 

Chege ambaye pia ni memba wa kundi la TMK Wanaume Family amesema kuwa licha ya kutokea kwa tukio hilo, hakupata majeraha makubwa zaidi ya kupata mtikisiko katika bega lakini baada ya muda afya yake ilitengemaa.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni miezi miwili tangu kutokea kwa ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa kiungo wa Simba, Patrick Mafisango maeneo ya karibu na chuo cha Ufundi Stadi (Veta), ikiwa ni mita chache kutoka sehemu ambayo Chege amepata ajali.

“Ajali imetokea jana (juzi) usiku majira ya saa tano, nilikuwa natoka Sinza naelekea Temeke, ndipo ghafla ilitokea pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa kasi na jamaa ambaye baadaye ilibainika kuwa alikuwa amelewa, ndipo tukakutana uso kwa uso, alivunjika mguu na majeraha mengine.

“Gari limeharibika sana sehemu ya mbele imefumuka, lipo Kituo cha Polisi cha Chang’ombe, pia kumbe jamaa alikuwa ameiba pikipiki hiyo ndiyo maana alikuwa kwenye kasi kubwa, nimeondoka asubuhi (jana) na sasa nipo Kigoma kwa ajili ya shoo ya Kigoma All Stars,” alisema Chege ambaye ni mwenyeji wa Kigoma.

No comments:

Translate