tangazo

Sunday, July 15, 2012

Wachunguzi wapata picha ya Tremseh

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria wamesema kuwa shambulio lilofanywa na serikali siku ya Alhamisi katika kijiji cha Tremseh inaelekea lililenga wanajeshi walioasi na wanaharakati wa upinzani. 


Wachunguzi hao walisema baada ya kuzuru kijiji hicho, kwamba jeshi lilitumia silaha nzito, kama mizinga, katika shambulio hilo.

Damu ilitapakaa kwenye nyumba zilizolengwa, na nyumba tano ziliteketezwa.

Upinzani ulisema mauaji hayo yalikuwa makubwa ambapo watu zaidi ya 200 waliuwawa, lakini hawakutoa ushahidi thabiti kuwa raia wengi wasiokuwa na silaha ndio waliouwawa.

Wachunguzi hao watarudi tena leo kwenye kijiji hicho kuendelea na kazi yao.

No comments:

Translate