tangazo

Tuesday, July 10, 2012

Mwakyembe ‘avamia’ Kituo cha Mabasi Ubungo

                                                                 Mh mwakyembe.


 WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amefanya ziara ya kushitukiza katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) na kusema, sekta hiyo inakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia usafirishaji nchini.

Mwakyembe alifanya ziara ya kushtukiza jana saa 11.00 alfajiri akitokea Dodoma anakohudhuria vikao vya Bunge, kwa kile alichoeleza ni kuitikia wito  kutoka kwa abiria mmoja aliyempigia simu juzi usiku na kumweleza kuwa  kunafanyika ulanguzi wa nauli kwa abiria.

Katika ziara hiyo, Dk  Mwakyembe aliyeongozana na maofisa wakuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Maofisa wa polisi wa Usalama barabarani, aliamuru magari yaliyokuwa yamezidisha  nauli kukamatwa na kutozwa faini ya Sh250,000 pamoja na kuwarejeshea kiasi cha fedha kilichozidi abiria wote.

“Ninachotaka mimi ni kila mtu kupata haki yake, wenye magari fanyeni biashara kwa kufuata taratibu zilizopo. Katika ziara yangu ya leo nimegundua katika sekta hii kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria taratibu na kanuni zinazosimamia sekta hii na nitafuatilia ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuhakikisha  tabia hiyo inakoma,” alisema Mwakyembe.

 Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji wa Sumatra ambao katika ziara hiyo waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Ahmad Kilima kutumia nusu ya muda wao ndani ya ofisi na nusu inayobaki nje ili kuhakikisha wanakamata  magari yote yanayokiuka taratibu ikiwamo la kuzidisha nauli kwa abiria.

Huku akipongezwa na abiria waliokuwa wakielekea mikoani kwa kusaidia kurejeshwa kwa  fedha zao, Dk Mwakyembe alisisitiza kuwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwamo yaa kuzidisha nauli ni wizi na inawaumiza wananchi ambao wengi wao ni masikini.

 “Nauli kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa basi la kawaida ni Sh45,000, kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga Sh31,400 ni nani kati yenu amelipa zaidi? alihoji  Dk Mwakyembe akiwa ndani ya moja ya mabasi yaliyokuwa yanayofanya safari  za kutoka  Dar es Slaam kwenda Mwanza. Kufuatia swali hilo, kundi la abiria walisimama na kuanza kuonyesha tiketi zao ambapo Waziri huyo aliamru konda wa gari hilo kuanza azi ya kurudisha fedha iliyozidi kwa abiria wake kabla ya kuruhusiwa kuondoka katika kituo hicho.

Pia Dk Mwakyembe aliamuru kila basi lililokutwa na kosa la kuzidisha nauli pamoja na matatizo mengine kutozwa Sh250,000 kwa kila kosa na kusisitiza kurudishwa kwa nauli za abiria.
 Katika ziara hiyo, Dk Mwakyembe aliwataja wamiliki kuwa wanachangia vitendo vya uvunjwaji wa sheria kwa kushishindwa kuwawajibisha wafanyakazi wao pindi inapotokea malalamiko kama hayo.
 Waziri aliwataka madereva kutii sheria za barabarani huku akisisitiza kwamba asimilia 75 ya ajali zinazotokea barabarani zinatokana na uzembe wa madereva.

 Kuhusu tatizo la madereva kutokuwa na mikataba alisema atalifanyia kazi, lakini akataka nao kuwasilisha malalamiko rasmi ofisini kwake ili aweze kuyafanyia kazi.  Adhabu kwa gari mbalimbali  Makosa mbalimbali yaliyojitokea jana mbele ya ukaguzi wa Waziri huyo wa uchukuzi ni makondakta kuzidisha nauli, mabasi ya safari ndefu kuwa na dereva mmoja, baadhi ya mabasi kuwa na leseni zilizokwisha muda wake na madereva kutokuwa na leseni.

 Abiria waliozungumza na Mwananchi walipongeza hatua ya Dk Mwakyembe kuvalia njuga suala hilo wakisema hatua hiyo inaweza
 kubadili tabia ya wafanya biashara kujihusha na vitendo vya ulanguzi wa nauli. Sumatra wanena
 Kwa upenda wake Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa (Sumamtra)   Kilima alisema ukaguzi wa jana ulihusisha zaidi mabasi yanayofanya inazofanya safari zake Dar es Salaam na Mwanza ambayo yalibainika kwa kiwango kikubwa kujijihusha na vitendo vya kutoza nauli kupita kiasi.

No comments:

Translate