tangazo

Thursday, July 19, 2012

MATUKIO YA UOKOAJI KATIKA AJALI ILIYOTOKEA ZANZIBAR YA KUZAMA KWA MV SKAGIT.

                        Waokowaji wakiwa wanaendelea na kuokoa watu katka meli boti ya kilimanjaro
                                        Muokowaji akiwa tayari kuiopoa maiti wa ajali ya Mv skagit
                                    Waokoaji wakiwa na baadhi ya majeruhi kwenye boti ya uokozi
                                    Raia wa kigeni wakiwa wanawasili bandalini baada ya kuokolewa

                  Majeruhi wakiwa wanapewa mablangeti ili kuizuia baridi ambayo imewapata
                         Majeruhi wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama jana katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31. 

Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.

SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar.

Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali.

No comments:

Translate