tangazo

Tuesday, July 17, 2012

Mubarak kurejeshwa jela


Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri, ameaumuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak kurejeshwa gerezani akisema kuwa hali yake ya afya imeimarika sasa.
 Mubarak, mwenye umri wa miaka ,84, alihamishwa kutoka gerezani humo mwezi jana baada ya ripoti za afya yake kuzorota .                                                                                              Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak                   
                                                                                                      

Alisemekana wakati huo kuwa alipatwa na kiharusi mwa mpigo na kuwekwa kwenye mashine ya kupiga moyo. Ripoti za Mubaraka kupoteza fahamu wakati huo zilipingwa vikali.

Mwezi Juni , Mubarak alihukumiwa kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya waandamanaji waliokuwa waanpinga utawala wake.

Mkuu huyo wa mashtaka, Abdel Maguid Mahmoud alitoa agizo la kumhamisha rais Mubaraka kutoka hospitali ya kijeshi ya Maadi hadi katika hospitali ya Tora baada ya afya yake kuimarika.

Naibu wa Mahmoud, Adel al-Saeed, ilisema kuwa jopo la madaktari lilikuwa hapo awali limesema kuwa afya ya rais huyo wa zamani iko sawa sasa mradi atumie madawa yake na kwamba kwa mtu mwenye umri wake hilo ni sawa.

Hata hivyo haikujulikana mara moja lini Mubaraka atarejeshwa tena gerezani.

Aidha mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa taarifa zozote kuhusu afya yake, wamisri wanazichukua kwa shauku kubwa.

Kumekuwa na shauku kubwa kuhusu afya ya Mubarak wengi wakisema kuwa taarifa zozote kuhusu afya ya

Mubarak zinatafsiriwa kama njama ya yeye kutaka kutolewa gerezani kwa misingi ya afya yake.

Hata hivyo wengi wanajua kuwa huu sio mwisho wa wao kusikia kuhusu sakata hii ya afya ya Mubarak.

No comments:

Translate