tangazo

Tuesday, July 17, 2012

FUPI za ENGLAND: RVP arudi Ze Ganaz, Vidic kurudi Man United Msimu mpya!

  RVP arudi Ze Ganaz, Vidic kurudi Man United Msimu mpya!



LIGI_KUU_ENGLANDWakati Nahodha wa Arsenal Robin van Persie amerejea London na kujiunga na Timu yake kwa ajili ya mazoezi huku kukiwa kuna kila dalili kuwa hana muda mrefu hapo Klabuni, Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic, ambae aliumia vibaya goti Mwezi Desemba, anaendelea vizuri na programu yake spesheli ya mazoezi na anatarajiwa kuonekana tena Uwanjani Msimu mpya wa Ligi Kuu ukianza.
RVPRVP1
Robin van Persie, ambae amechelewa kurudi mazoezini kwa sababu alikuwa akishiriki Mashindano ya EURO 2012 na Nchi yake Holland, jana alirudi kujiunga na Arsenal lakini bado kiwingu kimetanda kuhusu hatima yake kwa vile amekwisha tamka kuwa hataongeza Makataba wake na Arsenal Mkataba ambao umebakisha Miezi 12 kumalizika.
Dalili za kung’oka Van Persie zimeanza kuonekana baada ya Klabu ya Arsenal kutoitumia picha yake katika kutangaza Jezi zao mpya kwa Msimu ujao kwenye Jarida lao la Mtandaoni.
Staa huyo kutoka Uholanzi anahusishwa na kuhamia Klabu za Manchester City, Manchester United, Real Madrid na hata Juventus lakini hadi sasa hamna kilicho wazi kama atabaki Emirates au wapi atakwenda.
Hata hivyo, inategemewa uamuzi wa nini hatima yake utajulikana kabla ya Jumamosi wakati Arsenal wanatarajiwa kuondoka kwenda Kuala Lumpur, Malaysia ukiwa ni mwanzo wa Ziara yao itakayowachukua hadi China na Hong Kong.
Vidic
VIDIC_N_RIONahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic, ambae aliumia vibaya goti Mwezi Desemba anaendelea vizuri na programu yake spesheli ya mazoezi Kituo cha Carrington, Jijini Manchester, ambapo ndio mazoezi ya Man United hufanywa, na anatarajiwa kuonekana tena Uwanjani Msimu mpya wa Ligi Kuu ukianza.
Mechi ya kwanza ya Man United kwa ajili ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England ni hapo Agosti 20 watakapokuwa ugenini wakicheza Uwanjani Goodison Park na Everton.
Habari hizi njema kwa Wadau wa Man United zimetolewa na Maneja wao Sir Alex Ferguson ambae pia amethibitisha kuwa majeruhi mwingine, Chris Smalling, nae pia amepona nyonga na ataonekana Uwanjani Msimu ukianza.
Hata hivyo, Sir Alex Ferguson amekiri kuwa Beki wake mwingine Jony Evans, ambae alifanyiwa operesheni ya enka yake, huenda asiwe fiti kwa ajili ya Msimu mpya.
Hivi sasa Manchester United wapo kwenye Ziara huko Afrika Kusini na Jumatano Usiku watacheza Mechi na AmaZulu Uwanja wa Moses Mabhida Mjini Durban ikiwa ni moja ya sherehe za kuitukuza Mandela Dei, Siku ya kuzaliwa Shujaa Nelson Mandela ambae anatimiza Miaka 94.

No comments:

Translate