tangazo

Tuesday, July 17, 2012

Ukweli kamili kwa waliokufa kwa kunywa gongo.


                                                           Marehemu Banzi

                                                Jeneza lenye mwili wa Marehemu Banzi

                           Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Msiba wa marehemu Banzi.



                                                                 Marehemu Fikiri




                                                          Marehemu Hekima Bakari




                                                          Marehemu Mohamed Bakari


 UKWELI kamili kuhusu vifo vya watu sita waliokunywa gongo Kigogo Sambusa Luhanga Darajani, ambapo wengine wamelazwa wakiwa hoi katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam umebainika.
Gazeti hili limegundua kuwa gongo waliyokunywa ilikuwa ina mchanganyiko wa kemikali mbalimbali na dawa za viwandani na tayari sampuli yake imepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
Mteja mmoja ambaye kwa kipindi cha nyuma alikuwa ‘mnywaji mzuri’ wa gongo katika eneo hilo ambaye hakutaka atajwe gazetini alichambua jinsi pombe hiyo inavyotengenezwa.
Alisema kuwa kuna kemikali zinozotumika kutengezea konyagi ambapo watengenezaji wanazipata katika kiwanda kimoja (jina tunahifadhi) na wanachanganya na dawa nyingine.
Alibainisha kuwa kemikali moja hujazwa kwenye chupa ya ujazo wa lita moja na kuchanganywa na maji kiasi cha lita kumi kisha hutiwa spiriti pamoja na dawa ya madoa iitwayo ‘jick’ na mchanganyiko huo huzalisha kitu kinachoitwa gongo na kuanza kusambaziwa wateja.
Chanzo hicho kilisema kuwa njia hiyo ndiyo aliyokuwa akiitumia Hekima Bakari kwa muda mrefu, mama anayedaiwa kuwauzia gongo watu waliofariki na kulazwa Hospitali ya Amana.
Kiliendelelea kufafanua kuwa mama huyo ametengeneza mtandao na alikuwa akisambaza kinywaji hicho Gongo la Mboto, Kipunguni, Chanika, Kitunda, Kimara Bucha na Kigamboni.
Gongo hiyo ilianza kuua Jumatatu ya wiki iliyopita ambapo ilimuua Juma Abdallah baada ya kunywa kinywaji hicho na wanywaji wengine wakawa wanajificha kwa kuwa walikuwa wakiogopa kukamatwa na polisi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa katika eneo hilo la Kigogo Mbuyuni, Mohammed Mnunga aliwataka wote waliokunywa gongo hiyo kujitokeza na kwenda kupimwa afya zao kwa usalama wao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amepiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na kupika, kuuza au kunywa pombe haramu ya gongo na akasema tayari watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na sakata hilo.
Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kuwa ni Ramadhan Selestin (30), Salehe Omary (17), Shukuru Marungu (20), Charles Ibrahim (20), Fadhili Juma (20) wote ni wakazi wa Kigogo na Abdallah Mnazi (30) mkazi wa Tabata.
Aliwataja pia waliofariki katika nyakati tofauti kuanzia Julai 7 hadi 12, mwaka huu, katika maeneo ya Kigogo Mbuyuni kuwa ni Juma Abdallah (60), Mathew Roman (35), Khalid Hamis (31), Mohamed Said (25) na Antipal Raphel (60) wote wa Kigogo Mbuyuni na Hekima Bakari, ambaye ni muuzaji wa gongo hiyo.

No comments:

Translate