tangazo

Monday, August 27, 2012

Boko Haram kwenye mazungumzo na serikali



                                     Abubakar Shekau kiongozi wa kundi la Boko Haram

 Serikali ya Nigeria imeelezea kuanza mazungumzo na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la
Boko Haram kwa lengo la kujaribu kumaliza mashambulizi makali yanayofanywa na kundi hilo mara kwa mara nchini Nigeria.

Msemaji wa rais ameelezea kuwa mazungumzo yalikuwa yanafanywa kwa njia zisizo rasmi ingawa hakutoa maelzo zaidi.

Hata hivyo viongozi wa kundi hilo mwanzoni mwa wiki walielezea kuwa hawako tayari kwa mazungumzo ya amani na serikali.

Boko Haram,kundi ambalo linataka kuundwa kwa jimbo litakalofutuata sheria za kiisilamu , linatuhumiwa sana kwa kuua mamia ya watu na kisha kushambulia makanisa na maeneo mengine ya umma.

"mazungumzo yanayofanyika yanaendelea kwa faragha kwa lengo la kuelewa nini hasa matakwa ya kundi hili na nini hasa kinachoweza kufanyika kuhakikisha mzozo huu unakomeshwa" alisema msemaji huyo Reuben Abati.

Aliongeza kuwa lengo hasa la mchakato huu ni kutafuta amani na uwiano na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa thabiti.

Msemaji huyo aliongeza kuwa baadhi ya wanachama wa kundi hilo ndio wanaohusika na mazungumzo hayo. Boko Haram, ambalo maana yake ni kuharamisha masomo ya kigeni, linajulikana kwa vitendo vyake vingi vya kigaidi.

Kwa mujibu wa duru za habari nchini Nigeria, hili ndio itikio la kwanza rasmi la serikali ya Nigeria kuthibitisha kuwepo mazungumzo kati ya kundi hilo na maafisa wa serikali.

Juhudi za mapema za kufanya mazungumzo na kundi hilo ziligonga mwamba pindi zilipozungumziwa tu kuanza.

Nigeria imegawanyika hasa mara mbili, upande mmoja kwa waisilamu wengi wanaoishi maeneo ya Kaskazini na upande mwingine kwa wakristo wanaoishi maeneo ya kusini.

No comments:

Translate