tangazo

Saturday, August 25, 2012

TANZANIA YATAJWA KUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA MASUALA YA KUWAPOKEA WAKIMBIZI KWA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI.



         RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE


MAKAZI YA MUDA YA WAKIMBIZI NDANI YA BARA LA AFRIKA.


 TANZANIA yatajwa kuwa mfano wa nchi inayopokea wakimbizi na baadae kuwapatia uraia wa nchi hiyo wakati Uganda ikilaumiwa kwa kuweka sheria kali.

Ongezeko la wakimbzi katika mataifa mbali mbali ya bara la Afrika limepelekea serikali ya Kenya chini ya wizara ya sheria kuandaa mkutano wa siku mbili mjini Mombasa, kujadili changamoto zinazowakumba na namma ya kuimarisha  ushirikiano baina ya wakimbizi na wenyeji.

Wajumbe kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika mashariki na kati wanaoshiriki katika mkutano huo wamekubaliana kuhamasisha nchi zote husika ili kuanza kuondoa kasumba na unyanaypa  na kutomtizama kila mkimbizi  ni mhalifu au mwenye nia ya kufanya kitu kibaya ugenini.


Suala la ajira na rasilimali katika taifa linalowapokea wakimbizi limezungumziwa kuwa ni changamoto kuu hasa wenyeji wanapohisi kwamba wanatumia rasilimali zao pamoja na wageni.


Mfumo uliotumika na nchi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya congo-DRC kuwapokea wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi tangu mwaka 1971 umejadiliwa katika mkutano huu wa Mombasa.

Kenya ni moja wapo ya nchi inayowapatia hifadhi wakimbizi wengi, hasa kutoka Somalia, Ethiopia na Sudan Kusini, hata hivyo wale  wanaopatikana wanaingia nchini humo kinyume cha sheria wamekuwa wakiishia gerezani au kurejeshwa katika nchi wanazotoka licha ya kuwepo machafuko ya kisiasa yanayoendelea huko.

Wakati huo huo Tanzania imetajwa kama mfano mzuri katika nchi za kanda ya maziwa makuu iliyoleta mabadiliko makubwa kwa wakimbizi kwa kuwapa uraia. 


Huku Uganda ikisemekana kuweka sheria kali na kukosa kuwapa uraia wakimbizi walioishi  katika taifa hilo kwa miaka mingi.

No comments:

Translate