tangazo

Friday, August 17, 2012

Rooney ashangilia, asema sasa ni Rom + Roo






LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, aliyekuwa akisuasua kumuuza Robin van Persie kwenda Manchester United amekubali kwa dau la Pauni 24 milioni.

Arsenal ilithibitisha kukamilika kwa 'dili' hilo na mchezaji huyo amekwenda Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Klabu hiyo ilikubalia kuanzishwa upya kwa mazungumzo, na lengo ni kumchukua mchezaji huyo na sas Van Persie ni mchezaji halali wa United.

Alex Ferguson alisema, kumsajili mchezaji huyo, sasa itakuwa kazi kwa Manchester City kutetea taji lake.
Wenger alifanya kazi ya ziada kumshawishi Van Persie kubakia lakini ilishindikana na Van Persie alikuwa anataka kuondoka tu.

Kocha huyo wa Arsenal aliulizwa na Televisheni ya Ufaransa kama alikuwa na mpango wa kununua mchezaji mwingine: "Tayari tumeshanunua mchezaji, yuko [Lukas] Podolski na [Olivier] Giroud. Tunasikitika kumpoteza mchezaji mwenye ubora, lakini mkataba wake umebakia mwaka mmoja na hatuna jinsi."

Van Persie aliweka wazi katika taarifa yake ya Julai 4 kwamba anataka kutwaa mataji. Kwa njia nyingine, hafurahishwi na jinsi Arsenal FC inavyokwenda". Alikataa moja kwa moja kumwaga wino na alikuwa amebakiwa na miezi 12. Arsenal ilikuwa ikimtaka kwa udi na uvumba mchezaji huyo.

Taarifa ya Arsenal ilisema: "[Sisi] kama Arsenal tunathibitisha Robin van Persie amekwenda Manchester United. Van Persie anakwenda Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kabla ya kuanza mazoezi."

Arsenal ilitangaza Paundi 20 milioni kama bei ya kumuuza mchezaji huyo. Kabla ya kwenda nchi za Asia Julai 21, ambako Van Persie hakwenda na klabu ilipokea ofa kutoka klabu za United, City na Juventus, ambazo zote zilimtaka kwa Paundi 15 milioni.

Juzi United iliandika kwenye mtandao wake kuwa "Taarifa Mtu aliyekuwa na furaha alikuwa Wayne Rooney, ambaye alisema sasa safu yao ya ushambuliaji imekamilika.

"Van Persie ni mkali," Rooney alisema. "Amefanya makubwa akiwa na Arsenal kwa miaka mingi. Kuja kwake kutaongeza thamani ya timu na sasa itakuwa Rom + Roo."

No comments:

Translate