tangazo

Thursday, August 16, 2012

ROBIN VAN PERSIE AKUBALI KUJIUNGA NA TIMU YA MANCHESTER UNITED.

                                                             Robin Van Persie

MCHEZAJI Wayne Rooney wa Manchester United hivi sasa amepata pacha wake ambaye ni RVP, yaani Robin Van Persie ambaye usiku wa kuamkia leo amenunuliwa na klabu hiyo kwa mpunga wa Pauni milioni 22 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 54.3
RVP anatarajiwa leo kwenda Old Trafford kwa ajili ya vipimo vya afya yake na kusaini mkataba ambapo atakuwa akilipwa zaidi ya Pauni 200,000 kwa wiki ambazo ni sawa na Sh. Milioni 493.7
Kwa mujibu wa mtandao wa SunSport, kocha Fergie wa United anategemea kukamilisha uhamisho huo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Van Persie atakuwa mshambuliaji wa mbele ambapo Rooney atakuwa akimsaidia kwa nyuma.
Mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo baada ya kugombewa pia na Manchester City na Juventus ya Italia.
Mzee Wenger wa Arsenal alisema kwamba: “Inasikitisha sana kumpoteza mchezaji  muhimu kama huyo. Alikuwa bado ana mwaka katika mkataba wake hivyo hatukuwa na jinsi bali kumwacha aondoke.”

No comments:

Translate